Gazeti la Charlie Hebdo lapigwa marufuku Senegal
Senegal imepiga marufuku usambazaji wa jarida la Charlie Hebdo kote nchini humo. Nchi ya Senegal ni nchi ambayo asilimia kubwa ni waisilamu hivyo basi inadaiwa kuwa uamuzi huo umepokewa kwa furaha na wananchi hao.
Nchi hio pia ina uhusiano wa karibu na Ufaransa ambayo ilikuwa mkoloni wake na majarida mengi ya kifaransa yanapatikana nchini humo.
Jarida Charlie Hebdo limesambazwa kote duniani likuwa na kibonzo kinachomkejeli mtume akionekana kulia huku akishika bango linalosema ”Mimi ni Charlie” huku kichwa kinachofuata kikisomeka, ” Yote yamesamehewa”.