Friday, 30 January 2015

Chikawe: CUF walikaidi amri ndio maana walipigwa.

Chikawe: CUF walikaidi amri ndio maana walipigwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Chama cha CUF kilitimiza masharti yote lakini polisi ina haki ya kuzuia endapo itajiridhisha kuwa kuna uvunjifu wa amani.
Akifafanua Bungeni kuhusu wanachama wa  CUF kupigwa na Polisi,  Chikawe amesema CUF wakiongozwa na kiongozi wao walikaidi amri ya polisi, na ndiyo maana walipigwa. Katika tukio hilo lilitokea juzi    wanachama  wa  CUF walizuiwa kwa kipigo  wakati  wa maandamano  yalioyoongozwa  na  Mwenyekiti  wa  chama  hicho, Profesa  Ibrahim  Lipumba kuelekea Mabagala jijini Dares salaam
Kwa upande mwingine Waziri Chikawe   ameongeza kuwa CUF inatafuta umaarufu wa kisiasa na kusisitiza kuwa   Jeshi la polisi halitamuogopa,  kumhofia mtu,  na  amewaagiza polisi nchini kote kufanya kazi yao bila hofu wala kumuogopa mtu.

clouds stream