Rais wa Urusi, Vladmir Putin
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Ulaya
watakutana mjini Brussels kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kufuatia
mashambulizi ya Mashariki mwa Ukraine.
Mkutano huu wa dharula umeitishwa baada ya raia 30 kuuawa kwa
makombora, mauaji yaliyotekelezwa na Waasi wanaodaiwa waliungwa mkono na
Urusi na kushambulia bandari ya Mariupol wikendi iliyopita.
Majeshi ya NATO yamesema mamia ya vifaru vya Urusi, Magari ya Silaha
yalikua Mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi imekana kujihusisha moja kwa
moja na mashambulizi hayo.