Mourihno ataka kumsajili Gerald
Kocha mwenye majigambo ya hali ya juu nchini Uingereza Jose Mourihno akihojiwa na kituo kimoja cha radio nchini Uingereza ametoa maneno ya kejeli kwa nahodha Steven Gerard kwa kusema kuwa angemsajili nahodha wa Liverpool Steven Gerard kwa mkopo mwisho wa msimu kipindi ambacho Gerard atakuwa anaelekea klabu la Marekani LA Galaxy.
Kocha huyo aliongêa maneno hayo kuelekea kwenye mpambano wa nusu fainali ya Kombe la Ligi ambayo iliishia 1-1.
Mourihno ashangazwa kwa kitendo cha nahodha huyo kuikacha ligi ya Uingereza na kuelekea Marekani licha ya ubora alionao mchezaji huyo huku akikumbuka jinsi alivyomkosa kumsajili mchezaji huyo msimu wa 2005.