Saturday 17 January 2015

Ligi kuu Tanzania bara hapatoshi Kesho, Yanga, Simba, Azam kusaka pointi tatu

Kikosi cha Simba ambacho kesho kitacheza na Ndanda FC mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda.

Kindumbwe ndumbwe cha kugombania ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kinaendelea kesho Jumamosi baada ya kusimama kwa muda huku wawakilishi wa michuano ya vilabu ya Afrika , Azam FC na Yanga wakiwa viwanjani.
Yanga, ambao ni wawakilishi katika kombe la shirikisho Afrika, watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam wenye uwezo wa kuchukua watu 60,000 katika jitihada za kuwa kileleni.
Hata hivyo, haitakuwa rahisi kwa Yanga kuwafunga Ruvu ambao wapo nafasi ya pili katika msimamo wakiwa na pointi 16 kwa kuonesha ni moja kati ya timu ngumu. Yanga, ambao hivi karibuni walimrudisha kocha wao Mholanzi Hans Van der Pluijm, wapo nafasi ya 3 katika msimamo wakiwa na pointi 14.
Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la vilabu la washindi Afrika, Azam FC (nafasi ya nne katika ligi-pointi 14) , watakuwa uwanja wa Kambarage dhidi ya Stand United
Simba,mabingwa wa zamani, wakiwa na raha ya kushinda ubingwa wa kombe la Mapinduzi liliolisha hivi karibuni Zanzibar na rekodi isiyoridhisha katika ligi, watakuwa kusini mwa Tanzania (Mtwara) kupambana na wenyeji, Ndanda FC katika jitihada za kujinasua kutoka katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi tisa, baada ya kufanya vibaya hapo awali chini ya kocha aliyetimuliwa, Mzambia Patrick Phiri.
Mbeya City, ikiwana nafasi ya 13 katika ligi ya timu 14, watakuwa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania( Mwanza) kucheza na Kagera Sugar (yenye pointi 14) wakati Tanzania Prisons (ikiwa ya mwisho-pointi7) watacheza na Mgambo mkoani Tanga.
Viongozi wa ligi, Mtibwa Sugar ( pointi 16) ya Morogoro watakuwa dimbani Jumapili dhidi ya JKT Ruvu huku Coastal Union ya Tanga ikiikaribisha Polisi huko Tanga.

clouds stream