Wednesday, 7 January 2015

UN YATHIBITISHA PALESTINA KUJIUNGA ICC

UN YATHIBITISHA PALESTINA KUJIUNGA ICC



Umoja wa mataifa umethibitisha kuwa Palestina itakuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICC iliyo chini ya amri ya Roma kuanzia tarehe 1 mwezi Aprili mwaka huu.
Hii ni kulingana na taarifa kutoka kwa katibu-mkuu wa Umoja huo Ban ki-Moon, iliochapishwa katika mtandao wa mkataba wa Umoja wa Mataifa. Uwanachama wa ICC utaiwawezesha Palestina kufuatilia mashitaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Israeli katika siku zijazo.
Lakini pia utayawezesha makundi ya wapiganaji wa Kipalestina kushtakiwa. Rais wa Palestina Mahmoud Abass alituma maombi ya kujiunga na mahakama ya uhalifu wa kivita wiki iliyopita, jambo lililoikasirisha Israeli.
Hatua hiyo inajiri huku Marekani na Israel zikipinga hatua hiyo na kusema kuwa itachochea uhasama kati ya Israel na Palestina. Tayari Israel imesitisha fedha za kila mwezi za Palestina ambazo imekuwa ikichukua kama kodi kwa niaba yake.
Wiki iliopita waziri mkuu nchini Israel Benjamini Netanyahu alisema kuwa hatokubali wanajeshi wake kufikishwa mbele ya mahakama hiyo.

clouds stream