Bony avunja rekodi ya Toure, ghali zaidi Afrika
Mshambuliaji wa timu ya ligi kuu ya Swansea Wilfried Bony avunja rekodi ya Yaya Toure kwa kupata mzigo mrefu zaidi unaofikia paundi za kiingerereza 28M huku Yaya Toure akisajiliwa kwa Paundi 24M msimu wa 2010 aliposajiliwa akitokea Barcelona. Pia mali na mshahara Wilfried Bony ana bonus kwa kila mechi atakayocheza akiwa na Manchester City inayofikia paundi 20,000, Licha ya Bony kuungana na nahodha wake wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure hapo Manchester City ambao pia watakuwa pamoja kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika huko Guinea ya Ikweta.
Wilfried Bony alikuwa mfungaji bora kwenye msimu uliopita kwa kufunga magoli 20,ni bora zaidi katika kufumania nyavu ndio maana kila akisajiliwa anavunja rekodi ya usajili, alipojiunga na Swansea akitokea Vitesse Arnhem msimu wa 2013 pia alivunja rekodi ya klabu kwa usajili wa paundi 12M. Wachezaji wengine wa Afrika wanachukua mzigo mkubwa kwa sasa ni Emmanuel Adebayor,Samuel Etto na Didier Drogba.