Thursday, 29 January 2015

Islamic State waishambulia Misri, watu 26 wauawa Majeshi ya serikali ya Misri

Islamic State waishambulia Misri, watu 26 wauawa

Majeshi ya serikali ya Misri
Majeshi ya serikali ya Misri
Takriban watu 26 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic State Kaskazini mwa Misri katika eneo Sinai
Gari lililokuwa na mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini mwa Sinai katika mji wa El-Arish na kuwaua wanajeshi kadhaa. Mashambulizi mengine kama hayo yalifanyika katika mji jirani Sheik Zuwayid na mji wa Rafah katika mpaka wa Gaza.
Kundi la wapiganaji la Ansar Beit al-Maqdis ambalo ni mshirika wa wapiganaji wa Islamic State wamekiri kutekeleza shambulio hilo.
Maafisa wa jeshi nchini Misri wanasema gari hilo lililokuwa na mabomu liliegeshwa nje ya ngome ya jeshi ya El-Arish na mashambulizi yake yalilenga hoteli ya jeshi na maeneo mengine mhimu katika kituo hicho.
Hata hivyo kundi hilo lilianza kutekeleza mashambulizi yake nchini Misri tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais aliyekuwa na msimamo mkali wa Kiislam Mohammed Morsi mwaka 2013.
Hofu imetawala katika miji kadhaa nchini Misri wiki hii kutokana na sherehe za kumbukumbu za kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo na aliyeondolewa madarakani mwaka 2011 Hosni Mubarak.
Eneo la Kaskazini mwa mji wa Sinai kumekuwa na hofu ya mashambulizi ya kigaidi tangu mwezi Oktobar mwakajana ambapo wanajeshi kladhaa waliuawa katika shambulio.
Kundi hili la Ansar Beit al-Maqdis ambalo kuanzishwa kwake ilikuwa ni hamasa ya kundi la kigaidi la Al Qaeda, liliamua kubadili mtazamo wake na kuanza kutekeleza na kutii amri za kundi la wapiganaji wa Islamic state lililoshamiri Iraq na Syria, na malengo ya kundi hili ni kuhamasisha watu kuasi na kuuangusha utawala wa sasa wa Rais Misri Abdul Fattah al-Sisi.

clouds stream