Friday, 30 January 2015

LHRC yalaani Prof. Lipumba kudhalilishwa


LHRC yalaani Prof. Lipumba kudhalilishwa



Prof.Lipumba akiwa katika gari la Polisi mara baada ya kukamatwa juzi jijini Dar es salaam.
Prof.Lipumba akiwa katika gari la Polisi mara baada ya kukamatwa juzi jijini Dar es salaam.
Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimelaani kitendo cha jeshi la polisi kumpiga na kumdhalilisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba.
Akitoa tamko hilo lililokuwa katika sehemu ya maazimio katika kongamano la kujadili mapungufu ya katiba pendekezwa kwa wahaririri wa vyombo vya habari, asasi za kiraia na wanazuoni mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi. Hellen Kijo Bisimba amesema kitendo hicho hakivumiliki na kina lengo la kudhoofisha demokrasia na uhuru wa kikatiba katika kufanya maandamano.
Ameongeza kuwa  jeshi la polisi linatakakiwa kijitazama upya katika kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao vinginevyo  wanaendelea  kujenga chuki baina yao na wananchi kwa hila za kisiasa badala ya kuwa kimbilio la raia.
Katika hatua nyingine  katika mada iliyowasilishwa na aliyekuwa mjumbe wa bunge la katiba Bw. Hafley Polepole pamoja na kueleza katiba pendekezwa kuwa na mapungufu mengi ya kiuandishi na kisanifu amesema ni aibu kwa Tanzania yenye wasomi kuandika katiba kama hiyo huku akieleza sheria ya mabadiliko ya katiba kuwa nje ya muda wa kura ya maoni.

clouds stream