Thursday, 29 January 2015

Mgomo waendelea Kariakoo, Wananchi wakosa huduma

Mgomo waendelea Kariakoo, Wananchi wakosa huduma

Maduka yakiwa yamefungwa Kariakoo jijini Dares salaam leo
Maduka yakiwa yamefungwa Kariakoo jijini Dares salaam leo
Idadi ya watu yapungua Kariakoo kufuatia mgomo wa wafanyabiashara.
Idadi ya watu yapungua Kariakoo kufuatia mgomo wa wafanyabiashara.
Asilimia kubwa ya maduka yamefungwa kutokana na mgomo wa Wafanya biashara.
Asilimia kubwa ya maduka yamefungwa kutokana na mgomo wa Wafanya biashara.
Wananchi wakosa Huduma katika maduka ya Kariakoo kutokana na mgomo unaoendelea.
Wananchi wakosa Huduma katika maduka ya Kariakoo kutokana na mgomo unaoendelea.
Asilimia kubwa ya maduka yamefungwa leo kutokana na mgomo.
Asilimia kubwa ya maduka yamefungwa leo kutokana na mgomo.
Wafanyabiashara katika maduka ya Kariakoo jijini Dar es salaam wameendeleza mgomo  huku  asilimia kubwa  ya Maduka yakiwa  yamefungwa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari wa Mtandao wa Hivisasa  baadhi ya  wafanyabiashara hao wamedai kwamba wataendelea na mgomo hadi pale kiongozi wa wafanyabiashara hao atakapo achiwa  baada ya kukamatwa na jeshi la polisi jana.
Kwa mujibu  wa  Kaimu kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP), Simon Siro aliwaambia kuwa kiongozi wao alikamatwa na polisi mapema jana asubuhi na kusafirishwa kwenda Dodoma, ambako anadaiwa kutenda kosa la uchochezi.
Katika hatua nyingine wananchi  pamoja na wateja kutoka nje ya nchi wameiomba serikali kukaa na wafanyabiashara hao  ili kutatua mgogoro huo unaowasababishia kuingia gaharama wasizo zitarajia pamoja na nchi kukosa mapato.

clouds stream