Monday, 26 January 2015

Serikali yaanza ujenzi wa barabara za kupunguza foleni Dar

Serikali yaanza ujenzi wa barabara za kupunguza foleni Dar

Waziri wa Ujenzi Dkt Magufuli na viongozi wengine wa Dar es Salaam katika uzinduzi wa miradi ya barabara Dar es Salaam siku ya tarehe 26 Jan 2015
Waziri wa Ujenzi Dkt Magufuli na viongozi wengine wa Dar es Salaam wakiweom Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Mecky Sadick na wabunge wa Mkoa huo katika uzinduzi wa miradi ya barabara Dar es Salaam siku ya tarehe 26 Jan 2015
WIZARA ya Ujenzi imezindua miradi ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam zitakazogharimu sh.Trilioni moja.
Miradi hiyo ilizinduliwa leo na Waziri wa Ujenzi John Magufuli na kueleza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ambayo jumala yake ni kilometa 55.2 baada ya miaka mitatu suala la msongamano wa magari jijini itakuwa historia.
Barabara zilizozinduliwa ni ile ya Msewe –Baruti hadi Chuo kikuu cha Dares Salaam yenye urefu wa Km 2.6,Kigogo-Tabata km 1.6,Mbezi Mwisho Goba hadi Tangibovu km 9.,External Kilungule km 3,Wazo mapaka Goba km 20 na mbezi mwisho mpaka kinyerezi km 14.
Katika ziara ya uzinduzi huo, Magufuli aliongozana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,wabunge wa maeneo husika na kuhudhuriwa na wananchi wa maeneo hayo. Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo, Magufuli aliwataka wakandarasi kukamilisha miradi kwa muda uliopangwa na kutaka sualala msongamano wa magari hususa ujenzi wa barabara hizo uangaliwe kwa jicho la hurua kwa wabunge wa mkoa huo kuungana katika kutetea bungeni.
Alisema serikali ni tajiri hivyo ni lazima watalipa huku akiwataka wakandarasi wote kuendelea na kazi na kudai kwani watalipwa kwani wiki iliyopita wamepata fedha kadhaa toka hazina na wataendelea kupokea na kulipa wakandarasi.
“miradi hii inagharimu sh.Trilioni moja na baada ya miaka mitatu suala la msongamano litakuwa historia; tulichelewa kuanza kujenga barabara hizo lakini tumeanza na tutakamilisha “ Alisema
Magufuli na kuongeza kuwa katika kuhakikisha misongamano inakuwa historia ni lazima wakazi wote kuungana na kuzingatia sheria kwa kuacha kufanya biashara katika barabara za pembeni ikiwa ni pamoja na kila mmoja kuwa mlinzi wa barabara.
“kwa mfano barabara za mradi wa mabasi yaendayo; kazi zitakazokamilika mwezi Machi mwaka huu na kuanza kutumika. Sasa zinafanywa ni soko kwa wafanyabiashara, hilo ni kosa” Alisema Magufuli na kuwataka mkuu wa mkoa na viongozi wa siasa kuzingatia sheria kwa kuondoa wauza matofari, gereji mitumba na wengineo huku akieleza kuwa wananchi watambue ukubwa wa barabara ni mita 15 kila upande.
Wakati wa uzinduzi wa barabara ya Msewe, Magufuli alihaidi kujenga ukuta wa shule ya msingi Msewe huku Mbunge wa Ubungo John Mnyika akichangia madawati yenye thamani ya sh.milioni 10 toka mfuko wa jimbo, naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akitoa ahahdi ya CCM sh.milioni tano kwa ajili ya madawati shuleni hapo.
Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS). Patrck Mfugale alisema barabra zote hizo zinasimamiwa na Tanroads kwa uurefu wa km 55.2 na barabara za urefu wa km 27.2 zimeishaanza kujengwa.

clouds stream