Sunday, 31 July 2016

Lembeli Ajitosa Mkutano Wa Rais Magufuli Shinyanga

Tarehe Aug 01, 2016
Raqis Magufuli na James Lembeli.
Rais Magufuli na James Lembeli.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama, James Lembeli ameibuka katika Mkutano wa Rais, John Pombe Magufuli uliofanyika Mjini Kahama baada ya Rais Magufuli kumkaribisha na kumtaka arudi Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lembeli aliihama CCM na kuhamia CHADEMA mwaka jana na kugombea Ubunge Jimbo la Kahama na kuangukia pua.
Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi CCM na kusema kuwa kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza kitu, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.
Naye Lembeli amesema amekwenda katika mkutano huo kwa kuwa kazi inayofanywa na Rais Magufuli ndiyo ambayo amekuwa akiipigania alipokuwa Mbunge wa Kahama kwani rushwa imekithiri.
Aidha amerudia kauli yake aliyoitoa siku chache zilizopita na kusema kuwa hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama hicho akisafishe kabisa.

PICHA: Pale Usemi ‘Siasa Sio Uadui’ Unapodhihirika

Tarehe Aug 01, 2016
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Mh. Nape Nnauye na Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA wakijadiliana jambo wakati alipokutana katika shughuli ya kuaga mwanahabari Mpiga Picha Marehemu Joseph Senga aliyefaiki mwishoni mwa wiki hii Nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi ya moyo  shughuli hizo za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Senga zimefanyika Sinza na mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Kwimba mkoani Mwanza kwa mazishi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Mhe. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA (kulia) wakijadiliana jambo wakati alipokutana katika shughuli ya kuaga mwanahabari Mpiga Picha Marehemu Joseph Senga aliyefaiki mwishoni mwa wiki hii nchini India alipokuwa akitibiwa maradhi ya moyo. Shughuli hizo za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Senga zimefanyika Sinza na mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Kwimba mkoani Mwanza kwa mazishi.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Mh. Nape Nnauye akizungumza na Mh. Edward Lowasa Waziri Mkuu wa Zamani na kada wa CHADEMA katikati kushoto ni Kada mwingine wa CHADEMA Ndugu Khamis Mngeja.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Mhe. Nape Nnauye (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa (katikati). Kushoto ni Kada mwingine wa CHADEMA Ndugu Khamis Mngej

Wazungu Wamfata Mtanzania Aliyetengeneza Chopa

CmvplPZXYAA-E5n
Wakati Serikali ikipiga ‘biti’ kali sana kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa yeyote yule anayejidai kutengeneza helikopta, Raia wa kigeni (Wazungu) kutoka nchini Afrika ya Kusini wamemtembelea Mkazi wa Tunduma, Mkoani Songwe, Adam Kinyekile, 34, ambaye ametengeneza helikopta na kumpatia mwaliko maalum wa kwenda kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa hizo huko bondeni.
Hivi karibuni, Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake na kuunda helikopta ambayo ilivutia wengi sana na kupelekea Kiongozi wa Mwenge, George Mbijima akiwa Tunduma kumtembelea na kuweka jiwe la msingi katika eneo ilipo helikopta hiyo.
Ni dhahiri kuwa onyo la Serikali kupitia TCAA la kupiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na utengenezwaji wa chopa bila kufuata utaratibu lilimhusu Bwana Adam na pengine kumkatisha tama asiendelee na utengenezaji wa chopa hiyo na sasa wazungu wamekuja kumvuta na si ajabu chochote atakachokivumbua zaidi tutaambiwa kuwa ni wazungu ndio wavumbua na si mtanzania ten

Friday, 29 July 2016

MO Bado Yupo Sana Msimbazi, Ataka Kufanya Uwekezaji Wa Bilioni 20


Tarehe July 29, 201610
Aliyewahi kuwa Mdhamini wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohamed Dewji ‘MO’ amedai kuwa tatizo la klabu hiyo ni bajeti ndogo inayoifanya ishindwe kujipambanua vizuri mbele ya wapinzani wake wakuu, klabu za Yanga na Azam na kusema kuwa yupo tayari kufanya uwekezaji wa Shilingi bilioni 20 endapo wanachama wa klabu hiyo wataridhia.
MO ameyasema hayo leo katika kikao chake na waandishi wa habari na kudai kuwa kusuasua kwa klabu ya Simba kunachagizwa kwa kiasi kikubwa na ufinyu wa bajeti yake na kwamba kinachomvutia kufanya uwekezaji huo mkubwa kwa Simba ni mapenzi aliyonayo kwa klabu hiyo huku akijaaliwa kipato na Mwenyezi Mungu.
Amesema anaipenda Simba toka moyoni na kudai aliwahi kuidhamini miaka ya nyuma na kufanya vizuri sana katika michuano ya kimataifa na kila mwanamsimbazi anatambua hilo na kama atakubaliwa kufanya uwekezaji huo atajenga kiwanja bora cha mpira, hosteli, sehemu ya kufanyia mazoezi (gym), na kuajiri kocha mwenye viwango katika kipindi kifupi cha miaka mitatu tu.
“Tatizo ni bajeti na kutolea mfano bajeti ya Yanga akidai ni shilingi bilioni 2.5, Azam nao ni kiasi hicho hicho lakini kwa upande wa Simba hata nusu ya bajeti za wapinzani wao yaani shilingi bilioni 1.2 ni tatizo,” amesema.
Amefafanua kuwa ili klabu iweze kuleta ushindani mzuri ni lazima iwe na uwezo wa kununua wachezaji jambo ambalo limekuwa tatizo kwa klabu ya Simba.
“Ukitaka kushindana lazima uwe na uwezo wa kununua wachezaji lakini mnapotoa milioni 30 za usajili hatuwezi kushindana katika dirisha la usajili kwasababu wenzenu wanatoa zaidi ya hapo,” amefunguka.
Kauli hii ya MO inakuja huku zikiwa zimesalia siku chache tu klabu hiyo kufanya mkutano mkuu wa wananchama siku ya Jumapili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay ambapo pamoja na mambo mengine suala la uendeshwaji wa klabu hiyo na uwekezaji unaotaka kufanywa na MO yatatawala katika mkutano huo

Lowassa Awapa Mbinu Mpya Wanaomuunga Mkono CCM


Tarehe July 29, 2016Edward Lowassa.
Edward Lowassa. Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amewataka wale wote waliokuwa wanamuunga mkono lakini wamebaki Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushikamana naye na kumpatia taarifa kwa hatma ya nchi.
Mjumbe huyo Kamati Kuu CHADEMA, amewataka kuendelea kumuunga mkono na wenzake ndani ya CHADEMA.
Lowassa ameyasema hayo katika taarifa yake aliyoitoa akiwa anatimiza mwaka mmoja tangu alipojiengua kutoka CCM na kujiunga na CHADEMA.
Amesema ana furaha sana kutimiza mwaka mmoja tangu atoke CCM na kujiunga CHADEMA na kudai kuwa uamuzi ule haukuwa rahisi lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu alifanya uamuzi huo wa kihistoria kwa hatma ya nchi.
“Najivunia uamuzi ule kwani umewafungua macho watanzania walio wengi na kuimarisha demokrasia nchini na tangu nijiunge na CHADEMA nimewakuta viongozi na wanachama walio na moyo wa dhati wa kuliletea maendeleo Taifa lao kwa vitendo,” ameongeza.
Amedai kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko, sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na imezidi kuthibitika kuwa hawawezi kuyapata ndani ya CCM isipokuwa ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla.
“Nawahakikishia watanzania na wana UKAWA kwa ujumla kuwa sasa hivi nina ari, nguvu na hamasa kubwa kuliko wakati mwingine wowote ule,” amedai Lowassa.

Walichokisema ACT-Wazalendo Kuhusu Operesheni ‘Ukuta’


Tarehe July 29, 2016ACT-frr
Chama cha ACT­Wazalendo kimetoa neno kuhusiana na operesheni ‘Ukuta’ iliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kudai kuwa hawakubaliani na jambo hilo kufanywa na CHADEMA.
ACT­Wazalendo wametoa lao hilo la moyoni kupitia akaunti yao ya Twitter na kutaka wanasiasa wa upinzani kuungana na kupigana vita moja.
Juzi CHADEMA walitangaza operesheni Ukuta ambapo wamepanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima Septemba 1, mwaka huu kama njia ya kupinga baadhi ya mambo wanayoyaona kuwa wananyanyasika kwa kile wanachokiita udikteta. 
Tayari tamko hilo la CHADEMA limepingwa vikali na Msajili wa Vyama vya Siasa na kudai kuwa ni uchochezi utakaovuruga amani ya nchi huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikidai kuwa madai ya Chadema ni uongo mtupu uliojaa ubabaishaj

Mwigulu Atema Cheche Kwa Mchina Aliyemtesa Mtanzania


Tarehe July 29, 2016Raia wa China akitemsa mtanzania.
Raia wa China akitemsa mtanzania.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ametua mkoa wa Geita kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyodaiwa kufanywa na raia wa China wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro, Geit
Aidha kwa muda wa wiki moja sasa imeripotiwa kutokea hali ya sintofahamu katika mgodi huo ambapo Mfanyakazi mmoja Raia wa Tanzania ametajwa kuteswa na kufanyiwa vitendo ya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.
Katika Ziara hiyo Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la Mtanzania kuteswa na mwajiri wake, kipigo kilichosababisha kupoteza fahamu na siyo kifo.
Kufuatia Mtanzania kuteswa Nchemba alikwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ya kushitakiwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi lililosababishwa apigwe.
Katika mahojiano ya Waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo, Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhusika hasa wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na akiwapo gerezani.
Waziri huyo alimchukua kijana aliyeteswa na kwenda naye mgodini kuwasaka waliopiga na kumpa mateso makali,ambapo aliwabaini Watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na Mchina mmoja walioshirikiana kumpiga.
Katika hatua nyingine Nchemba ameagiza wahusika wakamatwe mara moja na akaondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akiwa na kijana anayedaiwa kumtesa mtanzania.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akiwa na kijana anayedaiwa kumtesa mtanzaniaBaadhi ya wachina ambao ni Wahamiaji Haramu.Baadhi ya wachina ambao ni Wahamiaji Haramu.

Thursday, 28 July 2016

Rais Magufuli Kuunguruma Kahama Jumapili Katika Mkutano Wa Hadhara


Tarehe July 28, 2016.Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, ambao pamoja na mambo mengine utalenga kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu amesema Rais Magufuli atawasili Mjini Kahama siku ya Jumamosi jioni na kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili, Julai 31, mwaka huu.
Amewataka wananchi wa Kahama kujitokeza kwa wingi ili kumlaki kiongozi huyo katika ziara hiyo muhimu ya Rais Magufuli.
“Lengo lake ni kuwapongeza wananchi wa Kahama kwa kumpa kura nyingi katika Uchaguzi uliomalizika mwaka jana,” amesema Nkulu.

Miaka Miwili Jela Kwa Kukashifu Au Kutumia Vibaya Vielelezo Vya Taifa


Tarehe July 28, 20161000px-Coat_of_arms_of_Tanzania Mpiga Chapa wa Serikali amesema ni kosa kisheria kutoa lugha chafu ya kukashifu au kuandika maneno yenye lengo la kudhihaki bendera au nembo yoyote ya Taifa kwani kosa hilo linaweza kupelekea mtuhumiwa kufungwa kifungo gerezani kisichozidi miaka miwili.
Akiongea Jijini Dar es Salaam, Mpiga Chapa wa Serikali, Kassian Chibogoyo amesema wananchi wote wanapaswa kuheshimu vielelezo vya Taifa ikiwemo wimbo wa Taifa na nembo ya Taifa.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya mwaka 1971 na Sheria ya Bendera ya Taifa ya mwaka 1962 na Sheria ya Ngao ya Taifa pamoja na Sheria ya Alama za Taifa, zinamkataza mtu yeyote kutumia bendera ya Taifa, ngao ya Taifa au nembo ya Taifa kinyume na ilivyokusudiwa,” amesema.
Kwa mujibu wa Chibogoyo, sheria hizo zinamkataza mtu yeyote kutumia bendera, nembo ya Taifa au kitu chochote kinachofanana na bendera au ngao ya Taifa kama alama ya biashara, shughuli za kitaaluma au kwenye maandiko yoyote yanayokusudia mauzo.
Hivi karibuni imekuwa ni jambo la kawaida kukuta wananchi wakiwa wameweka bendera za Taifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika vyombo vya usafiri kama magari binafsi, daladala na hata bodaboda ambapo baadhi ya vyombo hivyo ni vya biashara

Haya Ndiyo Majina Ya Wadaiwa Sugu Bodi Ya Mikopo


Tarehe July 28, 2016Wahitimu vyuo vikuu.
Wahitimu vyuo vikuu. Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB),imetangaza majina ya wadaiwa sugu ambao ambao mpaka hivi sasa hawajaanza kulipa mikopo waliochukua kipindi wanasoma.
Kwa mujibu wa Bodi hiyo wahitimu hao ambao majina yao yapo kwenye orodha wamevunja mkataba kutokana na sheria ya bodi hiyo No. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) sehemu ya 19 (1). Aidha, wanataarifiwa kwamba, kulingana na sheria hiyo ya bodi (HESLB) No. 9 ya 2004, Bodi imedhamiria kutenda yafuatayo:­
(i) Bodi itachukua hatua za kisheria kulingana na kipengele cha 19 (a) (1) cha sheria ya bodi.
(ii) Mdaiwa atapewa penati ya 5% juu ya ile 5% iliyokua ikitozwa kabla kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo.
(iii) Mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni zilizoingiwa na bodi.
(iv) Mdaiwa atawekwa kwenye ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.
(v) Mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa Serikali au udahili wa masomo ya juu k
(vi) Maelezo yao yatapelekwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani, kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi. 

Tuesday, 26 July 2016

Safari Ya Yanga ‘CAF’ Yaota Mbawa


Tarehe July 27, 2016Donald Ngoma katika moja ya mechi na Medeama jijini Dar es salaam.
Donald Ngoma katika moja ya mechi na Medeama jijini Dar es salaam.
Klabu ya Dar es Salaam Young Africans imekubali kipigo cha goli 3­1 dhidi ya Medeama kutoka nchini Ghana.
Kipigo hicho cha Yanga dhidi ya Medeama kimezidi kufifisha safari ya Yanga kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
Aidha, Magoli ya Medeama yamefugwa na Daniel Amoah dakika ya 7 na Abbas Mohammed aliyefunga magoli mawili dakika ya 22 na 37.
Kwa upande wa Yanga Simon Msuva ndiye aliyefunga goli la kufutia machozi kwa Yanga kupitia mkwaju wa penati dakika ya 24.
Kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kusalia na michezo miwili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria watakaocheza nyumbani na TP Mazembe ya Kongo watakaocheza ugenini

Majaliwa Atoa Siku 14 Kupata Mpango Kazi Wa Kuhamia Dodoma

Tarehe July 27, 20161
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma siyo siasa kama watu wanavyodhani bali ni utekelezaji wa maamuzi kamili na kwamba Serikali inakamilisha eneo la kisheria juu ya uamuzi huo na kutoa siku 14 kwa uongozi wa Mkoa wa Dodoma kukamilisha mpango kazi na kumkabidhi mapendekezo.
Majaliwa amesema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa, Serikali za mitaa, viongozi wa dini, wajasiriamali, wazee wa mji huo, wasafirishaji, wafanyabiashara, wakuu wa taasisi za elimu, za kifedha na watoa huduma mbalimbali katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Hazina ndogo Mjini Dodoma.
Amesema hapa tulipofika ni hatua ya utekelezaji wa pamoja na hakuna namna nyingine kwa sababu uamuzi umeshatolewa na kuwahakikishia kwamba suala hilo sio la kisiasa kwani kinachokamilishwa sasa ni eneo dogo tu la kisheria juu ya uhamishaji wa makao makuu kuja Dodoma na katika Bunge la Septemba sheria hii itapitishwa.
Waziri mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo pamoja na wadau wake wakae na kuandaa mpango kazi wa jinsi ya kupokea na kutekeleza uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ndani ya siku 14 mkoa na kumkabidhi mapendekezo yao ili yaweze kuingizwa kwenye mpango mkubwa wa Serikali kuu.
“Uongozi wa Mkoa, ukishirikiana na Ofisi yangu kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais TAMISEMI usimamie na kuyaratibu majukumu haya na ndani ya siku 14 nipate mapendekezo (proposal) ya kwanza na namna mtakavyoyatekeleza,” amesisitiza.
Amesema chimbuko la uamuzi wa kuhamia Dodoma na kuifanya kuwa Makao Makuu ya Serikali lilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo imeendelea kudumu katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 chini ya Ibara ya 151. 
“Napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wote wa Chama kwa kusimamia ndoto ya Baba wa Taifa ya kuhamishia Makao Makuu hapa Dodoma. Ni imani yangu kuwa wananchi wote mtaunga mkono uamuzi huu muhimu kwa Serikali yetu na wananchi kwa ujumla, amesema.

Basi La UDA Lagonga Treni Na Kuua Dar Es Salaam


Tarehe July 27, 2016 Basi la Uda liligonga Treni katika eneo la Gerezani.
Basi la Uda liligonga Treni katika eneo la Gerezani.

Basi la UDA linadaiwa kugonga Treni katika eneo la Gerezani Kariakoo jijini Dar es salaam na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine 40 wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zimebainisha kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo.



Basi la Uda linalodaiwa kugonga Treni jijini Dar es salaam.
Basi la Uda linalodaiwa kugonga Treni jijini Dar es salaam.

JK Adai Hataki Kujihusisha Na Siasa Tena


Tarehe July 27, 2016 
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani Bagamoyo baada ya kustaafu Uenyekiti CCM.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani Bagamoyo baada ya kustaafu Uenyekiti CCM. 

Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anataka kupumzika na hayuko tayari kufanya shuguli za kichama wala kiserikali isipokuwa kutoa ushauri katika shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kilimo na mifugo. 
Kikwete ameyasema hayo Mjini Bagamoyo katika sherehe za kumkaribisha nyumbani na kumpongeza ikiwa ni siku chache tu tangu kukabidhi uenyekiti wa CCM kwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa katika kipindi chake ameweza kuongoza na kuiacha nchi ikiwa salama na tulivu licha ya kupitia katika vipindi vigumu tofauti.

“Namshukuru Mungu kwani nchi iko salama na chama pia kipo imara hivyo nataka nipumzike nisijihusishe tena na masuala ya kisiasa au kiserikali kwani kwa sasa kuna viongozi wenye uwezo isipokuwa kama mkija kwa masuala ya kimaendeleo nipo tayari kufanya hivyo,” amesema Kikwete.

 Awali mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alisema kuwa watamuenzi Dkt. Kikwete kwa kujenga mnara wa kumbukumbu katika ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani takika mti wa Mkungu Maarifa mahali ambapo kwa mara ya kwanza alitangaza nia ya kuwania Urais.

Alichosema Zitto Kuhusu Serikali Kuhamia Dodoma


Tarehe July 26, 2016Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.


Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameunga mkono harakati za Serikali kutaka kuhamia Mkoani Dodoma mara baada ya Rais, Dkt. John Magufuli kutangaza azma hiyo mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, ameandika yafuatayo;
Katika kutekeleza dhana ya kuirudisha nchi katika misingi ya kuasisiwa kwake, katika kampeni zetu za uchaguzi wa mwaka 2015, tuliahidi kwamba, kama tungeshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, serikali ingehamia Dodoma mara moja. Aidha mgombea wetu wa urais aliahidi kwamba angekula kiapo cha urais mjini Dodoma.
“Tulienda mbali zaidi tukasema kwamba kulikuwa na haja ya kuzitawanya wizara katika mikoa mbalimbali ili kuiweka serikali karibu na wananchi na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika pande zote za nchi. Katika kutekeleza hili, kwa kuanzia, tukaweka nia ya kuihamishia wizara ya kilimo mkoani Mbeya, Wizara ya Nishati na Madini mkoani Mwanza na Wizara ya Utalii na Mali Asili mkoani Arusha,”  ameandika Zittto.
Ni katika msingi huu wa kisera tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake sahihi na wa kijasiri wa kuhamishia serikali Makao Makuu ya nchi Mjini Dodoma. Uamuzi wa kuhamishia serikali Dodoma ulifanywa miongo mine iliyopita lakini serikali ya CCM ilishindwa kuutekeleza kwa visingizio mbalimbali. Nchi kadhaa zilizokuja kujifunza kwetu namna ya kuhamisha makao makuu zilikwishatekeleza uamuzi huu wa kisera bila kigugumizi. Nchi mojawapo ni Nigeria iliyohamisha makao makuu yake kutoka Lagos kwenda Abuja.
“Tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kila mara atakapochukua maamuzi ya kisera tunayoamini kwamba yana maslahi mapana kwa Taifa. Hatahivyo, tutaendelea kutekeleza kwa bidii wajibu wetu wa kumkanya na kumkosoa pale tunapoamini kwamba maamuzi ya serikali yake hayana maslahi mapana kwa Taifa, ikiwemo kumnya na kukandamiza misingi ya Demokrasia na kufifisha utawala wa sheria,” amemaliza kuandika Zitto.

Jeshi La Polisi Lawasaka Wabunge 2 Chadema


Tarehe July 26, 2016Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Wabunge 2 wa Chadema wako matatani kufuatia kuitwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha na kutakiwa kuripoti kwa RCO kufuatia madai ya kufanya mikutano ya kisiasa suala ambalo limepigwa marufuku.
Wabunge walioitwa  kwa mahojiano   ni   mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo na  mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso.
Mwingine aliyeitwa ni  Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Jubilate Mnyenye na  Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta wote   wanadaiwa  kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.
Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.
Parreso alisema, walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane  lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.
Katika hatua nyingine  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.
Marufuku ya mikutano ya kisiasa imeendelea kuvikumba vyama vya Upinzani licha ya Jeshi la Polisi kusema kwamba halijapiga marufuku mikutano hiyo ya kisiasa.

Sumatra Yafungua Makucha,Yafutia Leseni Madereva Na Mabasi


Tarehe July 26, 2016Baadhi ya mabasi ya mikoani katika moja ya kituo cha mabasi nchini.
Baadhi ya mabasi ya mikoani katika moja ya kituo cha mabasi nchini.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesitisha leseni za madereva 18 kutokana na mgomo walioufanya kupinga wenzao kupelekwa mahakamani.
Aidha,Wamiliki wa mabasi 12 ambayo madereva hao walikuwa wanaendesha kwenda sehemu mbalimbali nchini, wamepewa siku saba kujieleza ni kwa nini wasifutiwe leseni za kutolea huduma hizo pamoja na kutakiwa kusitisha ajira kwa madereva hao.
Kwa mujibu wa  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alisema Julai 23 mwaka huu mkoani Kagera, madereva wa mabasi hayo walifanya mgomo kupinga kitendo cha madereva wenzao kupelekwa mahakamani, kukosa dhamana na kulala rumande kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ikiwamo kuendesha kwa mwendo kasi.
Kamanda Mpinga alisema dereva yeyote atakayeendesha gari kwa kasi ya zaidi ya kilometa 90 kwa saa atafikishwa mahakamani na sio kutozwa faini kama awali ili kuhakikisha matukio ya ajali yanapungua nchini.
Alisema kutokana na hali hiyo madereva wanaoendesha mabasi yanayoanza safari zake kwenye Manispaa ya Bukoba, walisitisha huduma kwa kushinikiza Mahakama iwaachie wenzao waliokamatwa kwa makosa ya mwendo kasi.
Naye Mkurugenzi wa Sumatra, Gilliard Ngewe, aliyataja mabasi pamoja na madereva waliositishiwa leseni kuwa ni Hussein Tegatega na Miraji Kondo wa Kampuni ya RS Express wanaoendesha basi lenye namba za usajili T 425 DDT aina ya Zongtong linalotoka Bukoba kwenda Dar es Salaam.
Said Omary na Amos Danney wa basi la Kimotico lenye namba za usajili T 966 CDY aina ya Nissan linalotoka Bukoba kwenda Arusha na madereva wanne wa mabasi ya Princess Muro yenye namba za usajili T 166 DCA na T 923 DCT yanayosafiri kutoka Bukoba kwenda Dar es Salaam.
Madereva hao ni Ally Mshuza, Twalibu Ondossy, Costa Andrew na Witness Lema.
Wengine  ni Musa Tindwa na Gerald Beti wa Kampuni ya Osaka Raha wanaoendesha basi lenye namba za usajili T 968 CPC linalofanya safari zake Bukoba kwenda Dar es Salaam na Paul Ngussa wa basi lenye namba za usajili T 810 BDW aina ya Scania linalotoka Bukoba kwenda Musoma, mali ya Kampuni ya Bunda Express.

Monday, 25 July 2016

Mvua Yatibua Dabi Ya Manchester



Tarehe July 25, 2016Manchester-United-Supporters
Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa.
Mechi hiyo ilikuwa imepangiwa kuchezewa uwanja waBirds Nest, Uchina na ingekuwa ya kwanza kwa mameneja wapya Pep Guardiola na Jose Mourinho.
Jumapili, Mourinho alikuwa amedokeza kwamba hali katika uwanja huo ilikuwa mbaya.
Hata kabla ya mechi kuahirishwa rasmi, Guardiola alikuwa amesema matumaini yake ni kwamba wachezaji wake wasiumie.
City na United wamesema “waandalizi wa mchuano huu pamoja na klabu zote mbili” wameamua kuahirisha mechi hiyo iliyopangiwa kuchezewa uwanja uliotumiwa kuandaa michezo ya Olimpiki 2008.
Mvua kubwa ilinyesha Jumapili na watabiri wa hali ya hewa walisema mvua zaidi ingenyesha Jumatatu.
United watarejea Manchester baadaye leo nao City wasafiri hadi Shenzhen Jumanne kwa mechi dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani siku ya Alhamisi.

Zitto Kushuhudia Hillary Clinton Akithibitishwa Mgombea Wa Democratic

Tarehe July 25, 2016Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe.
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameondoka nchini kuelekea Philadelphia nchini Marekani kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention) utakaomthibitisha Bi.Hillary Clinton kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis, akiwa kwenye Mkutano huo Zitto atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani pamoja na kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la Wanachama wa ACT Diaspora la nchini Marekani.

Aidha, pamoja na mambo mengine Zitto atakuwa na mazungumzo maalum na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad juu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar na Taifa kwa Ujumla.
Zitto na Maalim Seif ndio wanasiasa pekee nchini walioalikwa kwenye shughuli za chaguzi za nchini Marekani.

Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Septemba, Mawaziri Wengine Kufuata


Tarehe July 25, 2016Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote  hapa nchini kuhakikisha kuwa wanahamia makao Makuu ya Dodoma kama amri ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoitoa kwenye mkutano maalumu wa CCM.
Akizungumza kwenye maadhimisho  ya Mashujaa Kitaifa, yaliyofanyika mjini Dodoma Mhe Majaliwa amesema baada ya agizo la Rais alimuita Waziri wa nchi ofisi  ya Waziri mkuu pamoja na Katibu mkuu na kuwaagiza wakamilishe nyumba yake atahamia mwezi wa tisa mkoani Dodoma.
Amesema yeye akitangulia Dodoma mwezi wa tisa Mawaziri wengine wote wamfuate ikiwa ni kutii agizo la Rais Magufuli linalowataka watendaji wa serikali kuhamia Dodoma.
Amewasihi wana Dodoma kuwa serikali inafika Dodoma na kusisitiza kuwa utekelezaji wake anausimamia kwa nguvu zote.
Ametoa nasaha kwa wananchi kuhakikisha kuwa Dodoma inakuwa ni kisiwa cha amani, kuongeza uwekezaji katika mahoteli, Nyumba za kulala wageni na huduma nyingineno  kwa kuwa wageni wengi watafika mkoani humo kupata huduma mbalimbali za kiserikali.

Saturday, 23 July 2016

Magufuli Kukabidhiwa Uenyekiti CCM Leo, Fuatilia Live Hapa


Tarehe July 23, 2016Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Chama Cha Mapinduzi leo   kinatarajia kumpata Mwenyekiti mpya wa Taifa, Rais John Magufuli, katika Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Aidha, Tayari vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, vimeshapitisha kwa kauli moja jina la Rais Magufuli kugombea uenyekiti wa Taifa wa chama hicho.
Kwa mujibu wa  msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka alisema kikao hicho baada ya kupokea jina la Rais Magufuli kutoka Kamati Kuu, kimeridhia lipelekwe katika Mkutano Mkuu.
“NEC kwa kauli moja imepokea pendekezo la Kamati Kuu na kutafakari na kupitisha jina la Rais John Magufuli, kugombea uenyekiti wa CCM na kesho (leo), jina hilo litawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ili kuthibitishwa kwa kura za ‘Ndiyo”.
Katiba ya chama hicho ya mwaka 1997, inaeleza kuwa wakati wa uchaguzi unapofika, kazi mojawapo ya Nec ni kuteua jina la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa Taifa.
Katiba hiyo inasema pia kuwa unapofika wakati wa uchaguzi, kazi mojawapo ya Mkutano Mkuu wa Taifa ni kumchagua Mwenyekiti wa CCM.
Sendeka alifafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM, ili mtu aliyependekezwa kwa nafasi ya mwenyekiti wa CCM aweze kuchaguliwa, inabidi apate zaidi ya nusu ya kura za wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa.
Alisema kwa kuwa vikao vya juu vya Kamati Kuu na NEC ndivyo vilivyompendekeza Rais Magufuli kwenye nafasi ya uenyekiti na kwa kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuomba, wala kujaza fomu ya nafasi hiyo, basi kazi ya kumpigia kampeni itafanywa na chama chenyewe.
“Yeye hakuomba wala kujaza fomu, bali amependekezwa na NEC hivyo chama kitamsemea. Kitapita kwa wajumbe mbalimbali na kumuombea kura,” alisema.
Sendeka alisema kwenye ukumbi wa mikutano, wajumbe wawili wa NEC ndiyo watakaomwelezea na kumuombea kura kwa wajumbe ukumbini.
Kwa upande wa Mwenyekiti anayemaliza muda wake Dkt.Jakaya Kikwete alisema kumekuwa na maneno eti CCM itaishia mwaka 2020,lakini alisitiza kuwa CCM haitang’oka ng’o
Naye  Katibu mkuu Abdulrahman Kinana alisema idadi ya wajumbe wa NEC waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho ni 374, waliohudhuria ni 365 sawa na asilimia 97.5, hivyo akidi imetimia.
Fuatilia kila kinachojiri katika mkutano huo hapa hapa Hivisasa.co.tz pamoja  na Sasa Tv.

Askari Barabarani Auawa Kwa Kupigwa Risasi Akiongoza Magari



Tarehe July 23, 2016
trafik1
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku wa kuamkia leo  kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.
Amesema kwa sasa wanafanya kazi kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini na wahusika ni watu gani ili upelelezi wao uweze kuanza maramoja.

Friday, 22 July 2016

Samatta Atupia Kwa Penati Jana



Tarehe July 22, 2016Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
Mshambuliaji  wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ amefunga penalti ya tatu timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji  ikishinda kwa penalti 4-2 dhidi ya wenyeji Buducnost usiku huu Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica, Montenegro katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya mchujo wa kufuzu hatua ya makundi ya Europ League.
Timu hizo zilifikia kwenye matuta baada ya sare ya jumla ya 2-2, Genk ikianza kushinda 2-0, mabao ya Neeskens Kebano kwa penalti dakika ya 16 na Samatta dakika ya 79 Alhamisi iliyopita na usiku huu Buducnost wamelipa kisasi kwa ushindi wa 2-0.

Vyuo Vikuu 6 Vyapigwa ‘Pini’ Kudahili Wanafunzi 2016/17


Tarehe July 22, 2016udom-660x330
Serikali imevizuia kwa muda jumla ya Vyuo Vikuu sita nchini kutofanya udahili wowote kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Vyuo hivyo ni pamoja na Interntaional Medical and Technological University (IMTU) ambacho haviruhusiwi kudahili wanafunzi katika kozi zote, St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS) kozi zote, University of Bagamoyo (UoB) kozi zote, St. Joseph University College of Engineering (SJUCET) kozi zote.
Vingine ni University of Dodoma (UDOM) ambacho hakitaruhusiwa kudahili wanafunzi wa kozi ya udaktari, na State University of Zanzibar (SUZA) ambacho hakitaruhusiwa kudahili wanafunzi wa kozi ya udaktari.

Thursday, 21 July 2016

JK Arusha ‘Dongo’ Kwa Waliodhani CCM Ingemfia Mikononi



Tarehe July 21, 2016
Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM anayeondoka katika wadhifa huo, Dkt. Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM, Mjini Dodoma.
Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM anayeondoka katika wadhifa huo, Dkt. Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC), Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayeondoka madarakani, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amerusha dongo kwa wale wote waliofikiria kuwa chama hicho kingemfia mikononi mwake.
Kikwete ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua na kuongoza kikao chake cha mwisho kama Mwenyekiti cha Kamati Kuu (CC) na kuwakebehi wale wote waliodhani kuwa chama hicho kingeanguka kipindi cha uongozi wake.
Amesema waliodhani CCM ingekufa katika uongozi wake na kujiandaa kutoa salamu za rambirambi, basi imekula kwao.
“Wapo wale waliodhani kwamba wangeibuka lakini hawakuibuka na kamwe hawataibuka,” Amesema Dkt. Kikwete.
Wanachama wa CCM wapo Dodoma katika Mkutano Maalum utakaofanyika Julai 23, mwaka huu huku Rais, Dkt. John Magufuli akitarajiwa kuchukua hatamu ya uongozi wa CCM Taifa akimpokea Dkt. Kikwete.

Vigogo 3 MSD Waponea Chupuchupu 1 Aking’olewa


Tarehe July 21, 2016
Taasisi ya MSD.
Taasisi ya MSD.
Vigogo 3 kati ya 4 waliotumbuliwa mnamo tarehe 15/2/206 na Waziri wa Afya, Manedeleo ya Jamii Jinsi na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(Mb) wameponea chupuchupu kung’olewa katika taasisi hiyo ya MSD.
Vigogo hao ambao ni wakurugenzi walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.
Wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja  Bw.Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bw. Joseph Tesha, Mkurugenzi Ugavi Bw. Misanga Muja  na Mkurugenzi wa Ununuzi Bw.Heri Mchunga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Wadhamini imebanisha kuwa baada ya kufanya uchunguzi  Bw. Heri Mchunga ameonekana hana kosa hivyo amerudishwa kazini pamoja na kuhamishiwa kurugenzi ya ugavi kuwa Mkurugenzi.
Bw. Joseph Tesha naye amerudishwa kazini huku akitenguliwa ukurugenzi na atasubiri kupangiwa kazi nyingine.
Mwingine ni Misanga Muja aliyekuwa mkuurugenzi Ugavi amerejeshwa kazini huku akitenguliwa nafasi yake hivyo atakaa benchi kusubiri kazi nyingine.
Aliyetumbuliwa ni Cosmas Mwaifwani kufuatia Bodi hiyo kubaini kuwa ana makosa katika utendaji wake hivyo utendaji wake umesimamishwa kuanzia tarehe 8/7/2016.

China ‘Yamwaga’ Trilioni 16 Ujenzi Wa Kisasa Reli Ya Kati


Tarehe July 21, 2016
Usafiri wa Reli Tanzania.
Moja ya Treni ya abiria hapa nchini.
Benki ya Exim ya China imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Bilioni 7.6  sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati hapa nchini kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) unaotarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha.
Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 20 Julai, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, kuwa pamoja na kutoa fedha hizo zitakazofanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli ya kati benki hiyo itashirikiana na Tanzania  katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshaji wa reli.
Kwa mujibu wa taarifa ya kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imebainisha kuwa Pamoja na kukubali kutoa fedha hizo, Rais huyo wa Benki ya Exim ya China amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa dhamira ya dhati ya kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuharakisha ujenzi wa reli ya kati na ameahidi kuwa benki yake itatoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha mradi huo na miradi mingine ya maendeleo.
“Kuhusu huu mradi wa reli ya kati tuna mtazamo chanya, tunauona ni mradi mzuri na tutatoa ushirikiano wowote utakaohitajika. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania mchakato wa utekelezaji wa mradi huu utafanyika kwa mafanikio na kwa kuzingatia muda” Amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang kwa kukubali kutoa fedha hizo na amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kutekeleza mradi huo ambao tayari ujenzi wake umepangwa kuanza katika mwaka huu wa fedha kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi Trilioni 1 zilizotengwa katika bajeti.
Rais Magufuli amebainisha kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Congo.
“Kwa hiyo kukubali kwao ambako ilikuwa ni kitu kikubwa, inaonesha kwamba juhudi za Tanzania kwenda haraka haraka zinakubalika kimataifa, na wenzetu hawa wachina wana pesa nyingi.
“Na kule kuaminika kwamba tunakopeshwa kwa masharti nafuu, riba yake ni ndogo na huku kwetu ni mafanikio makubwa, kwa hiyo mizigo mingi tutakuwa tunaisafirisha, tutaendeleza reli yetu na bandari zetu” Amesema Rais Magufuli.
Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es salaam-Tabora-Isaka-Mwanza, Tabora-Mpanda-Kalemela, Tabora-Uvinza-Kigoma na Isaka-Keza-Msongati.
Mazungumzo kati ya Rais Magufuli na Rais wa benki ya Exim ya China yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.

Wednesday, 20 July 2016

Adhabu Kwa Wasaliti CCM Haikwepeki-Kinana


Tarehe July 20, 2016Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema wasaliti wote ndani ya chama watapata adhabu yao kulingana na kiwango cha makosa yao.
Amesema adhabu hizo zitaanzia kwa wale waliokisaliti chama hicho na kusaidia upinzani hasa katika uchaguzi uliopita huku wengine wakiyumba katika misimamo yao na kushindwa kusaidia wengine katika kampeni.
Inaaminika kuwa baadhi ya makada wa chama hicho walitetereka pale aliyekuwa anawania ruhusa ya chama hicho kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa kuamua kung’atuka na kuhamia upinzani baada ya jina lake kukatwa.
Inadaiwa kuwa alipoonda CCM, Mbunge huyo wa zamani wa Monduli na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliacha mtikisiko mkubwa miongoni mwa wanachama kati ya wale waliokuwa wanamkubali na wale wasiomkubali na kuibua mijadala ya ushabiki ndani ya chama hicho hadi kupelekea vigogo wengine kama Makongoro Mahanga na Balozi Mwapachu kujiengua kutoka CCM.
Hatahivyo muda mfupi baada ya uchaguzi kuisha Balozi Mwapachu aliamua kurudi CCM na kudai kuwa alifanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi.
Inaaminika kuwa wapo wengine ambao walitetereka na kukisaliti chama hicho hivyo ni suala la muda tu hadi pale tutakapojua ni nani na nani hasa wametumbuliwa kwa kukisaliti chama tawala.

Serikali Kununua Rada Mbili Kusaidia Ukusanyaji Wa Mapato


Tarehe July 20, 2016Radar-hatzerim-1-1
Radar-hatzerim-1-1
Serikali imetangaza kununua rada mbili mpya kwa ajili ya kusaidia kukusanya mapato zaidi ya Shilingi bilioni 18 ambazo zinapotea kila mwaka kutokana na kukosekana udhibiti katika anga la Tanzania.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Teknolojia, Edwin Ngonyani,  amesema hayo katika mkutano uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya anga pamoja na wamiliki wa kampuni za ndege barani Afrika.
Amesema katika awamu ya kwanza, Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya kununua rada mbili ambazo zitafungwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere na Kilimanjaro (KIA), huku awamu ya pili ikifungwa katika viwanja vya Mwanza na Songwe.
“Serikali tayari imeshatenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inanunua rada mbili, ili kuokoa kiasi cha takribani shilingi bilioni 18 ambazo zimekuwa zikipotea kila mwaka, jambo ambalo linafanya nchi kupoteza mapato, kwani inakuwa haiwezi kulisimamia anga lake lote na hivyo kufanya ndege, hata zile zisizotua nchini huku zikitumia anga hilo, kushindwa kulipa ushuru,” amesema.
Kwa sasa Kenya na Rwanda ndiyo nchi zenye rada hizo licha ya kuwa nchi hizo ni ndogo ukilinganisha na Tanzania.
Kwa upande wake, Mkurungezi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA), Hamza Johari, amesema kuwa ununuzi wa rada hizo utasaidia kuongeza mapato na hivyo kufanya viwanja vya ndege kujiendesha vyenyewe bila kusubiri msaada kutoka serikalini.
Mkutano huo ulikuwa ukikutanisha wamiliki wa ndege zilizokidhi vigezo na wadau mbalimbali wa masuala ya anga kutoka Bara la Afrika, ukiwa na lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

Wanafunzi 382 Warejeshwa UDOM


Tarehe July 20, 2016udom
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema wanafunzi 382 pekee kati ya 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum katika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) ndio wenye sifa za kurejea chuoni hapo ili kuweza kuendelea na masomo.
Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi  ilikiagiza Chuo cha Dodoma kuwarudisha nyumbani wanafunzi wa  Stashahada za Elimu (Sayansi, Hisabati na Teknolojia) kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na Tatizo la ufundishaji wa Stashahada hizo chuoni hapo.
Hatahivyo sakata hilo la wanafunzi hao kurudishwa liliibua mijadala ya kitaifa na bungeni huku baadhi ya wabunge wakiomba miongozo kutaka suala hilo lijadiliwe kama jambo la dharura baada ya wanafunzi hao kupewa masaa machache kupotea katika chuo hicho.
Akizungumza bungeni kutoa taarifa ya Serikali, Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako alisema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya walimu waliokuwa wanawafundisha wanafunzi hao kugoma kufundisha kwa muda wa mwezi mmoja.
Hatahivyo Rais Magufuli alisema baadhi ya wanafunzi hao hawakuwa na sifa stahiki na wale wasiokuwa na sifa kuwaita ‘vilaza’ huku akiahidi kuwa wanafunzi hao wataangaliwa upya na wale wenye sifa watarejea kuendelea na masomo yao.

clouds stream