Thursday, 31 August 2017
RAIS MAGUFULI ASITISHA BOMOABOMOA YA NYUMBA ZAIDI YA 300
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Rais Magufuli amesitisha zoezi la bomoabomoa la nyumba zaidi ya 300.
Nyumba hizo ni zile zilizojengwa katika Bonde la Makamba, Kata ya Tuangoma, Wilayani Temeke.
“Serikali imesisitiza kuwa zoezi hilo linapaswa kufanywa kwa kufuata taratibu na sheria,” amesema.
Hivi karibuni, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza Bomoa Bomoa nchi nzima kwa wananchi waliovamia na kujenga kando ya Mito na Bahari ikiwa ni siku chache baada ya kucha vilio maeneo kadhaa ikiwemo pembezoni mwa Barabara ya Morogoro eneo la Kimara na kuwaacha baadhi ya watu bila makazi.
Akizungumza Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema wananchi waliofanya makazi katika maeneo hayo wanapaswa kuondoka kabla ya kuvunjiwa kwa nguvu.
Bodi Ya Mikopo Yaongeza Muda Wa Kuomba Mikopo.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imeongeza muda wa maombi ya kuomba mkopo kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo wa 2017/2018.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, wanafunzi wa elimu ya juu sasa wataweza kuomba mkopo hadi kufikia Septemba 11, ikiwa ni siku saba mbele ya iliyokuwa tarehe ya mwisho hapo awali ya Septemba 4, mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema hadi kufikia jana, jumla ya waombaji 49, 282 wamekwishaingiza taarifa zao katika mtandao wa HESLB kwa ajili ya kuomba mkopo.
Kamanda Mambosasa Akemea Kauli Ya ‘Order’ Kutoka Juu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa katika uongozi wake hakutakuwa na kauli ya ‘order’ kutoka juu kutoka kwa askari polisi.
Kamanda Mambosasa amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na IGP, Simon Sirro kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam akitokea Dodoma alipokuwa Kamanda wa Polisi Mkoani humo.
Amesema mtu yeyote atakayesikia kauli ya ‘order’ kutoka juu, aikatie rufaa kwa kumpigia simu na kumueleza kuwa kuna mtu anataka kuchezea uhuru wake.
“Ukisikia askari anasema ‘order’ kutoka juu, ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji asiyejua kile anachotenda,” amesema.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni na miongozo inayoongoza jeshi hilo.
Watoto 4 Watekwa Nyara Arusha, Wazazi Watakiwa Kutoa Pesa
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Jiji la Arusha limeingia katika ‘headlines’ kuanzia siku ya jana baada ya kuripotiwa kwa matukio ya utekaji watoto wadogo huku watekaji wakidai pesa kiasi cha milioni 4 ili kuwaachia.
Inadaiwa kuwa tayari watoto wanne wametekwa, na watekaji hao wanatumia njia ya karatasi iliyoandikwa kwa kalamu na mkono kuwasiliana na wazazi wa watoto hao na kudai pesa ili kuwaachia.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahalifu hao na kuwatia nguvuni huku akiwataka wananchi kuwa watulivu.
Tuesday, 29 August 2017
Zitto: Siwezi Kukubali Uteuzi Wowote Wa Rais Magufuli
Rais Dkt. John Magufuli (kushoto) akiwa na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe (kulia).
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka na kudai kuwa hawezi kukubali uteuzi wowote ule kutoka kwa Rais Magufuli kushika nafasi yoyote ile.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amedai kuwa kukubali uteuzi kutoka kwa Rais Magufuli kutamnyima nafasi ya kujenga chama chake cha ACT.
Hivi karibuni Rais Magufuli alishangaza wengi pale alipoamua kuteua watendaji wawili katika Serikali yake kutoka chama cha ACTWazalendo, ambao ni wapinzani baada ya kumteua aliyekuwa Muasisi na Mshauri wa ACT Wazalendo, Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Siku chache baadaye Rais Magufuli alimteua aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na aliyegombea Urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Msukuma Amvaa Tundu Lissu Sakata La Wanasheria Kugoma
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amejitokeza na kupinga wito wa mgomo ulioitishwa na Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Lissu siku ya Jumapili alitoa wito kwa Mawakili wote ambao ni Wanachama wa chama hicho kususia shughuli za Mahakama ili kushinikiza Jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika na tukio la kulipuliwa ofisi za IMMMA Advocates zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.
Msukuma amesema kitendo cha Chama cha Mawakili kutangaza mgomo ni kutowatendea haki wateja wao kwa siku zote watakazoamua kususia shughuli za Mahakama.
”Watanzania kwa pamoja tunalaani kitendo kilichofanywa kwenye Ofisi za IMMMA Advocates kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kihalifu.Tunamuomba IGP Sirro afanye juu chini kuhakikisha watu hawa wanakamatwa.”Alisema Msukuma.
“Nilishtushwa sana na matamko yaliyotolewa na Rais wa TLS, Tundu Lissu kwamba anatangaza mgomo wa Wanasheria kuanzia kesho na keshokutwa. Najiuliza kama Tundu Lissu anatangaza mgomo wa Wanasheria, hiyo ndiyo hukumu ya kumpata mvamizi? Alihoji Msukuma.
Monday, 28 August 2017
POLISI: WALIOLIPUA OFISI ZA MAWAKILI WALIJIDAI KUWA MAASKARI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.
Walinzi hao wanadaiwa kukutwa baadaye maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.
Imedaiwa kuwa kundi lililobaki liliingia katika ofisi hizo hilo na kuweka vilipuzi vilivyotengenezwa kienyeji, ambavyo vililipuka muda mfupi baada ya watu hao kuondoka eneo hilo na kusababisha uharibifu wa wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.
Jeshi hilo limesema kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu waliofanya tukio hilo na kujua dhamira yao ili wafikishwe katika vyombo vya sheria kwani wajibu wa jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao na kamwe haliwezi kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi .
Aidha, jeshi hilo limewaomba waathirika wa tukio hilo na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio hilo.
Thursday, 24 August 2017
MMOJA AFARIKI , WENGINE WAKIJERUHIWA BAADA YA DALADALA KUGONGA TRENI NA KUBURUZWA
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya, wakiwemo wanafunzi, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kwenda shule kugonga Treni, eneo la Tanesco, Mkoani Morogoro na kuburuzwa umbali unaokadiriwa kuwa mita 150, Mkoani Morogoro.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Morogoro, Frank Jacob athibitisha.
Ndugu msomaji endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi juu ya tukio hili kadiri zitakavyotufikia kutoka mamlaka husika.
Lukuvi Ajibu Lawama Za Sumaye Kunyang’anywa Mashamba
Fredrick Sumaye.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi amesema mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu tosha ya kunyang’anywa ardhi hiyo pamoja na kufutiwa hati ya umiliki kwa kuwa anaingizia hasara serikali.
Waziri Lukuvi amefunguka hayo ikiwa imepita siku moja tangu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Fredrick Sumaye kudai chanzo cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM na kwenda kuupa nguvu upinzani, akielekeza lawama zake kwa Rais Magufuli na Waziri Lukuvi.
“Kila mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya ardhi ni sababu tosha ya wewe kunyang’anywa shamba lako au ardhi unayomiliki,” amesema Lukuvi.
Amesema kuna tabia imejitokeza kwa watu wachache kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi kuliko hata uwiano wa uendelezaji wa ardhi hiyo, kwa mfano kuna hati moja hapa ambayo inapigiwa kelele tokea mwaka 1939 imekuwa ikitembea mikono mwa watu.
“Sasa miaka ile watu walikuwa wachache unapokwenda kuchukua ardhi ya kijiji hekari elfu 60 kwa mfano hivi sasa wananchi utakuwa umewaachia kitu gani?” amehoji Mhe. Lukuvi.
Amesema imekuwa kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi maeneo huwa wanakimbilia kuchukua sehemu zenye manufaa makubwa kwa upande wao na mwishowe wanashindwa kuendelezaa maeneo hayo kama walivyoyakimbilia.
“Unawahi kuchukua sehemu zenye manufaa kama mto, ardhi inayolimika, sasa unachukua hekari zote hizo halafu huliendelezi mwishowe shamba hilo hilo tunalikuta Benki umelikopea fedha. Kisha umepata fedha hizo unakwenda kujengea ‘apartment’ sehemu nyingine na kule wananchi wanalimezea mate.Serikali wanatumia nguvu kubwa sana kutuliza wananchi wasivamie hilo shamba, halilimwi, serikali hatupati kodi,” ameongeza Lukuvi.
Kwa upande mwingine, Waziri Lukuvi amesema serikali imekuwa na huruma kwa miaka mingi kwa wananchi wake lakini serikali ya uongozi huu wamekubaliana kila mtu afuate sheria kama inavyotakikana.
UINGEREZA YAIPATIA TANZANIA TRILIONI 1 KUENDELEZA MIRADI YA MAENDELEO
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Serikali ya Uingereza leo imetoa Dola Milioni 450 (Sawa na Trilioni 1 za Kitanzania) ili kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Tuesday, 22 August 2017
Everton yaivuta shati Man City nyumbani
Wayne Rooney amefikisha jumla ya magoli 200 katika ligi kuu ya nchini England
Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Man city,imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton.
Everton almaarufu kama The Toffes, ndio walianza kuzifumania nyavu za Man City, kwa goli lilifungwa na mshambuliaji Wayne Rooney, Rooney amefikisha idadi ya magoli 200 katika michezo ya ligi kuu nchini England.
Katika dakika ya 82 Man City, walisawazisha goli hilo kupitia kwa winga Raheem Sterling aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Everton, Jordan Pickford.
Raheem Sterling akipiga shuti lililokwenda moja kwa moja nyavuni
Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kubakia na wachezaji kumi baada ya beki wa City Kyle Walker, na kiungo wa Everton Morgan Schneiderlin, kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kila mmoja kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Hali Ya Bulaya Yazidi Kuzorota, Akimbizwa Muhimbili
Mbunge wa jimbo la Bunda-mjini, Esther Amos Bulaya.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Mh. Joyce Sokombi amesema hali ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh. Ester Amos Bulaya imezidi kuwa mbaya.
Mh. Sokombi amesema pamoja na kwamba amepelekwa katika hospitali ya mkoa Mara Mbunge huyo hajapata nafuu, hivyo amepewa rufaa ya kuja hospitali kuu ya Taifa Muhimbili.Ester Bulaya alipata matatizo ya presha na kukimbizwa hospitali hapo jana huku akiwa kizuizini, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe alisema wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Tarime.
Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini
Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.
Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.
Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.
Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari wa kitamadunia.
Friday, 18 August 2017
Mkapa Kushuhudia Kagame Akila Kiapo Leo
Rais. Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Mteule wa Rwanda, Paul Kagame anatarajiwa kula kiapo cha Urais leo baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika Agosti 4, mwaka huu kwa asilimia 98.
Miongoni mwa viongozi wa Afrika watakaohudhuria sherehe hizo za kula kiapo ni Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye yupo nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo kusuluhisha mzozo wa kisiasa.
Sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Amahoro, zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali.
Kagame atakuwa anaanza muhula wa kwanza wa miaka saba tangu taifa hilo lilipofanyia marekebisho katiba yake.
Viongozi wengine watakaohudhuria sherehe hizo ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Rais wa Niger, Mahaadou Issoufou, Rais wa Senegal, Macky Sally, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Congo Brazaville, Sassou Ngueso
Thursday, 17 August 2017
Real Madrid yailaza Barcelona na kushinda kombe la Super Cup
Real Madrid yailaza Barcelona na kushinda kombe la Super Cup
Kwa mara nyengine Real Madrid imeilaza Barcelona 2-0 katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu na kuibuka mshindi kwa jumla ya mabao 5-1 na hivyobasi kushinda kombe la Super Cup.
Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya walitawala mechi hiyo licha ya kutoshoriki kwa nyota wao Cristiano Madrid.
Marco Asensio ambaye pia alifunga katika ushindi wa mechi ya kwanza huko Barcelona aliwapatia mabingwa hao uongozi wa mapema kupitia mkwaju wa maguu 25.
Karim Benzema aligusa kwa uhodari pasi nzuri iliopigwa na Marcelo na kumwezesha Samuel Umtiti kufunga bao la pili huku ikiwa wazi kwamba Barcelona wasingeweza kusawazisha.
Real Madrid ilicheza mechi hiyo kwa urahisi mkubwa huku Barca wakifanya mashambulio kupitia Lionel Messi na Suarez yaliogonga mwamba wa goli.
Akiwa kocha wa timu hiyo kwa miaka miwili pekee Zinedine Zidane ameiongoza Real Madrid kushinda mataji mawili ya vilabu bingwa na taji la La liga la 2016-17.
Na kufuatia ushindi huo ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa timu nyengine kuwabwaga mabingwa hao msimu huu.

Bi Mugabe aomba kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi
Mugabe na mkewe
Serikali ya Zimbabwe imemuombea mkewe Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini , maafisa wa polisi wa taifa hilo wamesema.
''Grace Mugabe alikuwa bado yupo Afrika Kusini'' iliongezea wakipinga ripoti za awali kwamba alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.
Mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 amemtuhumu bi Mugabe kwa kumshambulia katika hoteli moja mjini Johannesburg.
Polisi walitarajia kwamba bi Mugabe angejiwasilisha kwao mwenyewe siku ya Jumanne lakini hakufanya hivyo.
''Serikali ya Zimbabwe imewasilisha ombi la kumlinda kidiplomasia'', wizara hiyo ilisema katika taarafa yake.
SERIKALI YATOA TAARIFA YA AWALI KUUNGUA SOKO LA SIDO MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ametoa pole kwa wafanyabiashara wote walioathirika na janga la moto baada ya soko la Sido kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Mhe. Makalla soko la Sido lilianza kuungua saa 21:32 jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko hilo.
Pamoja na kutoa pole amewashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano kwa kazi kubwa ya kudhibiti moto huo usiendelee na kuleta madhara makubwa zaidi.
“Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya imeunda kamati ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha moto huo. Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana,” amesema Mhe. Makalla.
Aidha, amesema kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu au kikudi cha watu.
“Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu,” amesisitiza Mhe Makalla.
Monday, 14 August 2017
Uchaguzi Kenya: Raila Odinga awashauri wafuasi wa upinzani kususia kazi Jumatatu
Kinara wa muungano upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amewashauri wafuasi wake kususia kazi siku ya Jumatatu kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne iliyopita.
Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga amedai kuwa serikali ilikiwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani kabla ya kutangazwa matokeo.
Hii ni siku moja baada wa watu kadha kuripotiwa kuuawa maeneo tofauti ya mji wa Nairobi na Kisumu, wakati wafuasi wa upinzani walijitokeza kulalamikia matokeo ya uchaguzi
Wafuasi wa upinzani wakiandana mtaa wa Mathare Nairobi
Aidha Odinga amesema kuwa siku ya Jumanne, mrengo wa Nasa utatangaza mwelekeo ambao utachukua.
Bw Odinga baadaye alizuru mtaa wa Mathare Kaskazini jijini Nairobi ambapo msichana wa miaka tisa alifariki baada ya kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raia Odinga akipata kura 6,762,224.
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, alikuwa ametoa wito kwa Bw Odinga kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.
Wafuasi wengi wa Bw Odinga walihudhuria mkutano huo uwanja wa Kamukunji mtaa wa Kibera, Nairobi
Polisi wa kupambana na ghasia mjini Kisumu
Bw Annan alikuwa mpatanishi mkuu baada ya ghasia kuzuka baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 uliokumbwa na utata.
"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," amesema Dkt Annan kupitia taarifa.
"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi awali."
Mwaka 2007, watu zaidi ya 1,000 walifariki na wengine 600,000 wakafurushwa makwao wakati wa ghasia za kikabila zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)