Tuesday, 24 October 2017

Afande Sele Ammwagia Makonda Sifa Lukuki Kwa Hili, Adai Mengine Hayamuhusu






Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop, Afande Sele ameibuka na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makondakwa kitendo chake cha kuyakusanya magari mabovu ya askari na kwenda kuyakarabati.

Rapa huyo amesema kitendo cha mkuu huyo kimeonyesha taswira tofauti na kusema kuwa zamanimagari ambayo yalikuwayanachakaa yalikuwa yanauzwa kwa watumishi wa jeshi hilo kwa bei ya kutupa lakini yeye ameamua kufanya tofauti.

“Ingekuwa zile siku za zamani kidogo haya magari aliyoyakarabati huyu mkaka wa Dar wangeuziana mabosi wapolisi na wapendwa wao kwa shilingi laki mbili kila moja kama vyuma chakavu,” ameandika Afande Sele katikaukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

“Katika hili huyu jamaa wa Dar anastahili kongole lakini yale mengine mimi hayanihusu bora nikae kimya kwanzakwetu sio Dar,” ameongeza Afande Sele.

Mhe. Makonda hivi karibuni alikabidhi magari ya kisasa 18 kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa kwa ajili ya kusaidia kupambana na uhalifu na kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dar es Salaam.

Magari hayo ni kati ya yale 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu kwaajili ya kufufuliwa upya.

clouds stream