Monday, 16 October 2017

Mwanafunzi Aua Wenzake 5 Na Mlinzi Kwa Risasi






Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amewaua wenzake watano katika Shule ya Sekondari Mchanganyiko ya Lokichogio na mlinzi mmoja kwa kuwapiga risasi na baada ya kusimamishwa masomo shuleni hapo.

Akithibitisha tukio hilo, Kamishna wa Kaunti ya Turkana Seif Matata amesema mmoja wa wauaji ni mwanafunzi aliyekuwa amesimamamishwa masomo shuleni hapo kutokana na utovu wa nidhamu

Mwanafunzi huyo ajulikanaye kwa jina la Abrahamu wa kabila la Toposa kutoka Sudan Kusini,
aliyeshirikiana na watu wengine watatu kufanya ukatili huo anadaiwa kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu baada ya kusikika akitoa vitisho kuwaatakuja kuichoma shule hiyo kwa moto ili kulipa kisasi.

Siku ya tukio, mwanafunzi huyo akiambatana na wengine watatu alikuja asubuhi na kumuua mlinzi kisha kuelekea kwenye bweni la wavulana ambako ndipo alihisi wanafunzi waliomsababishia kufukuzwa shule walikuwa wakilala kisha kuhamia bweni la wasichana na kuwajeruhi wengine kadhaa.

clouds stream