Sunday, 15 October 2017

Uchaguzi Liberia: Weah na Boakai kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais

George Weah and Joseph Boakai composite image
George Weah (kushoto) na Joseph Boakai

Nyota wa zamani wa soka George Weah na makamu wa rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Liberia.

Karibu matokeo yote kwenye uchaguzi wa siku ya Jumanne yamehesabwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Bw. Weah ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la kandanda la Ballon D'Or, anaongoza kwa asilimia 39 huku Bw. Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29.

Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mwezi ujao.

Wanaongoza wagombea wengine 20 ambao wanataka kuchukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa rais barani Afrika na mshindi wa tuzo la amani la Nobel.

Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza.

Meneja wa zamani wa Bw. Weah akiwa mcheza kandanda, Arsene Wenger, mapema wiki iliyopita alipotoshwa na habari kuwa Weah tayari alikuwa amechaguliwa rais.

Kutana na wagombea wakuu

George Weah, 51:
Mshindi wa zamani wa tuzo la mchezaji bora  duniani wa Fifa.

Arsene Wenger, ambaye sasa yuko Arsenal,  alikuwa  kocha  wake huko Monaco miaka ya 1990.

Anaungwa mkono kisiasa na mbabe wa vita aliye  gerezani  rais wa zamani Charles Taylor.

Mke wa zamani wa Taylor Jiwel Howard  mgombea  mwenza wa Weah.

Joseph Boakai, 73:
Amepewa jina "Sleepy Joe".

Anakana hilo kwa sababu mara nyingi huonekana kwenye  kamera akisinzia.

Makamu wa rais wa Ellen Johnson Sirleaf tangu mwaka 2005.

Amejitenga na rekodi yake Sirleaf akisema  mengi   yanahitaji kufanywa.

clouds stream