Monday, 9 October 2017

RAIS MUSEVENI ATAKA WANANCHI KUFANYA KAZI SANA KULIKO KUSALI



Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni



Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amewataka wananchi wake kutumia muda mwingi kufanya kazi zaidi kuliko kusali ili kuliletea maendeleo taifa hilo.
Rais Museveni amesema hayo alipokuwa katika hafla ya “Uganda’s 19th National Prayer Breakfast” kwenye Hoteli ya Africana Jijini Kampala iliyoandaliwa na bunge la nchi hiyo.
Kiongozi huyo anayehisiwa kuwa na zaidi ya miaka 75 anataka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo akiwa
ameitawala Uganda kwa zaidi ya miaka 30 tangu aingie madarakani  mwaka 1986, akisaidiwa na vikosi vya Jeshi la NRA.
Hatahivyo, Katiba ya nchi hiyo hairuhusu mtu mwenye umri wake huo kugombea Urais naili kumuwezesha Rais Museveni aweze
kugombea, chama tawala kimpeleka muswada bungeni ili kufanya marekebisho ya Katiba ya Uganda.

clouds stream