Monday 30 October 2017

NECTA YAONYA WANAFUNZI WASIMAMIZI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE UKIANZA LEO

Image result for wanafunzi

Wanafunzi katika moja ya shule ya sekondari nchini.



Baraza la Mtihani nchini (NECTA) limesema halitosita kumchukulia hatua mwanafunzi yeyote pamoja wasimamizi wa Mitihani hiyo
ambao watakiuka sheria za mitihani ya kidato cha nne ambayo inaanza leo saa mbili za asubuhi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa (NECTA), Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandishi, ambapo amesema
Baraza hilo linatoa wito kwa kwa wasimamizi wa mitihani wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu.

“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatuakali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa” amesema Dkt Msonde.

Amesema Baraza hilo linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi
kuingilia majukumu ya wasimamizi.

Aidha,katika mitihani huo jumla ya watahiniwa 585,938 wamesajiliwa kufanya mtihani huo, ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kujitegemea ni 62,425.

“Kati ya watahiniwa wa shule 323,513 waliosajiliwa ,wanaume ni 159.103 sawa na asilimia 49.18 na wanawake ni 164,410 sawa
na asilimia 50.82,huku watahiniwa wenye uono hafifu ni 305 ambapo maandishi yao yanakuzwa”amesema Dkt Msonde.


clouds stream