Monday 2 October 2017

Afariki Dunia Akijazwa Dawa Ya Nguvu Za Kiume Kwa Pampu Ya Baiskeli

Image result for waganga wa kienyejiUpungufu wa nguvu za kiume umetajwa kuendelea kushika kasi miongoni mwa Wanaume hivyo kupelekea baadhi ya watu

kutumia dawa zisizostahili na kupata madhara makubwa Ikiwemo kifo.

Upungufu wa nguvu za kiume ni nini?
Upungufu wa nguvu za kiume ni kitendo cha mwanaume kushindwa kusimamisha uume na pia kushindwa kuendelea kubaki imara wakati wa tendo la ndoa.

Kutokana na tatizo la nguvu za kiume, Mwanaume aitwaye Joseph Sahani (60) mkazi wa kijiji cha Nzonza kata ya Salawe tarafa
ya Nindo wilaya ya Shinyanga amefariki dunia akiongezewa nguvu za kiume kwa mganga wa kienyeji Robert Nkoma (58) kwa
kujazwa dawa kwenye tundu la uume kwa kutumia pampu ya baiskeli.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Simoni Haule ambapo amesema tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 10 jioni.

“Chanzo cha tukio ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na kuamua kwenda kwa mganga
huyo ili atibiwe ndipo mganga akatumia njia ya kumuingiza unga unaosadikiwa kuwa ni dawa ya kienyeji kwenye tundu la uume
kwa kutumia pampu ya baiskeli akawa anapampu kama anajaza upepo na kusababisha marehemu kuishiwa nguvu na kutoka
damu nyingi kwenye uume na kusababisha kifo chake”, ameeleza Kamanda Haule.

Kamanda huyo ameongeza kuwa tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo ili afikishwe Mahakamani.

Kutokana na kuzagaa mabango ya wanganga wa Kienyeji wakijinasibu kutibu upungufu wa nguvu za kiume,asilimia kubwa
wamekua wakiwatapeli wagonjwa kwa kuwa dawa hizo wakati mwingine zinaua kabisa nguvu za kiume ulizokuwa nazo hapo
awali.

Inashauriwa kuwa endapo una upungufu wa nguvu za kiume muone Daktari kwa ushauri wa kitaalamu pamoja na tiba.

clouds stream