Sunday, 8 October 2017

WATOTO WANUSURIKA KIFO WAWILI WAKIJERUHIWA BAADA YA GARI KUGONGA TRENI




Watoto kadhaa wamenusurika kifo leo huku wawili kati yao wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga treni,eneo la Kwaminchi Mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, ajali hiyo ilitokea baada ya gari hilo kuzima ghafla katikati ya barabara ya treni ‘reli’ na kugongatreni hilo.

Watoto hao wanadaiwa kunusurika kifo baada ya kuruka kutoka katika gari hilo huku treni hiyo ikiwa inakuja kwa kasi.

clouds stream