Monday, 2 October 2017

Hamas na Fatah wasuluhisha tofauti

Viongozi wa Hamas na FatahViongozi wa Hamas na Fatah




Vyama viwili vikubwa vya siasa vya Palestina, Fatah na Hamas vimepiga hatua katika kusuluhisha tofauti baina yao iliyodumu kwa muongo mmoja, baada ya ziara iliyofanywa na Waziri mkuu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Rami Hamdallah ameuambia umati wa maelfu ya watu kwamba wakati umefika sasa kumaliza mgawanyiko mongoni mwa Wapalestina.
Mwezi uliopita chama cha Hamas kilikubaliana kuvunja utawala wao ukanda wa Gaza kwa ajili ya kupisha serikali ya muungano na chama cha Fatah kinachoongozwa na Waziri mkuu Hamdallah, ambacho makao yake ni Ukingo wa magharibi.
Akizungumzia hilo, kwa upande wake mjumbe wa Umoja wa Mataifa ukanda wa Gaza Nickolay Mladenov amesema serikali mpya ya Gaza imeweza kubeba majukumu yake, hali inayotia matumaini kwamba shida za kibinadamu zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

clouds stream