Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo yuko nchini Uganda kwa ziara rasmi .
Haijajulikana lengo la safari yenyewe lakini huenda inauhusiano na usalama wa mji mkuu wa nchi hiyo wa Mogadishu unaozidi kuzorota huku Uganda ikiwa na askari wengi kama walinda amani.Ziara hii inafanyika wiki moja tu baada ya kutokea shambulio kubwa la kigaida nchini Somalia ambalo limesababisha vifo vya mamia ya watu.
Shambulio hilo ndilo baya sana kuwahi kutokea mjini Mogadishu kwani takriban watu 358 wanaripotiwa kuaawa na wengine kujeruhiwa huku 56 hawajulikani waliko.
Rais Museveni wa Uganda
Ingawa haijulikani lengo la safari hiyo, lakini wachambuzi wanahisi ziara hii inaweza kuwa ni moja wapo ya jitihada za Somalia kuomba usaidizi zaidi wa kijeshi kutoka Uganda hasa ikizingatiwa kwamba, Uganda ni miongoni mwa nchi zinazochangia wanajeshi wake Somalia.
Hata hivyo, swali ni je, iwapo wataongezewa nguvu inaweza kuleta tofauti yoyote? kwa sababu hivi sasa tayari Uganda ina idadi kubwa zaidi ya wanajeshi Somalia.
Uganda inachukuliwa kama mshirika wa karibu na Somalia na kuafuatia shambulio hilo rais Museveni alililaani vikali.
Hakusema ni hatua gani Museveni angefanya kuweza kuzua shambulio kama hilo lakini Uganda ina vikosi zaidi nchini Somalia vikiwa chini ya kivuli cha vikosi vya kulinda amani vya Muungano wa Afrika.