Tuesday, 10 October 2017

Uchaguzi Kenya: Nini kitatendeka baada ya Odinga kujiondoa?

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu je uchaguzi utafanyika au mgombea aliyebaki Rais Uhuru Kenyatta atangazwe kuwa mshindi bila kufanyika uchaguzi.

Tayari Rais Uhuru Kenyatta amesema pamoja na kujiondoa Raila Odinga wa NASA uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.

Katika kupata ufafanuzi zaidi kuhusu utata huo Mwandishi wetu Idris Situma amezungumza na Dkt Alutalala Mukhwana ambaye ni mwanasheria aliyebobea katika masuala ya Kikatiba.

clouds stream