Tuesday, 10 October 2017

SERIKALI YAMJIBU DANGOTE



Aliko Dangote.



Serikali kupitia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage imemjibu Mfanyabiashara, Aliko Dangote
aliyenukuliwa akilalamika kuhusiana na Sera za Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na Uwekezaji nchini akidai kuwa
zinawaogopesha wawekezaji.
Waziri Mwijage amesema kuwa mfanyabiashara huwa hafahamu sheria zilizopo nchini na zinazoongoza sekta ya uwekezaji.
“Dangote hajui sheria zetu zinazoongoza sekta ya uwekezaji nchini na ndio maana ni rahisi kwake kuongea hayo aliyoyasema,” amesema Waziri Mwijage.
Dangote ambaye amewekeza katika kiwanda cha kutengeneza saruji Mkoani Mtwara amesema kuwa sera za Rais Magufuli
zinawatisha wawekezaji na kwmba si jambo zuri kwani mmoja akitishwa na wengine watakimbia.
Dangote ameweka wazi hayo katika kongamano lililofanyika Mjini London, na kusema sheria mpya zinazoundwa Tanzania
zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

clouds stream