Tuesday 10 October 2017

IGP SIRRO ATANGAZA VITA NA MANGE KIMAMBI


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema Jeshi lake linatambua makosa ya kimtandao ya nayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na linashughulikia suala hilo.
IGP Sirro amesema hapo Mjini Iringa mbele ya waandishi wa habari na kudai kuwa jeshi hilo linatambua uvunjifu wa sheria ya
makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ikiwemo kutoa machapisho mbalimbali ya matusi na
kashfa kwa serikali na viongozi wake lakini kwa sasa hawezi kusema ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwadada huyo anayeishi nje ya nchi.
Mange Kimambi ni mwadada, Mtanzania aishiye nchini Marekani, ambaye ni maarufu kwa kundi kubwa la watu watumiao mitandao
ya kijamii hasa mtandao wa Instagram.
Umaarufu wake unachagizwa na tabia yake ya kuelezea kwa uwazi bila kificho mambo yawahusuyo watu maarufu wakiwemo
wanasiasa, wanamuziki, wasanii wa filamu na hata wanamichezo, wakati mwingine kwa kashfa na matusi na wakati meingine
akiwasifia kadiri anavyoona yeye.
Moja ya tukio ambalo Mange Kimambi alilifanya hadi kusifiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe ni kuhamasisha
Watanzania waishio nje ya nchi kuchangia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu aliyepigwa risasi Mjini
Dodoma.

clouds stream