Sunday 23 November 2014

SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII


SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII



Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Sakata la wizi wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya Escrow watuhumiwa wote kujulikana wiki hii siku ya jumatano na Alhamisi. Katika siku hizo Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linatarajia kujadili ripoti ya escrow.
Hivi sasa  Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo ili kuokoa mabilioni ya fedha za wananchi zilizoibwa na watendaji wa serikalini na hatimaye kugawana.
Aidha,  katika Kikao cha Kamati ya Uongozi  wa Bunge  kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja  kama  iliyokuwa imepangwa awali.
Kwa upande mwingine   kambi Rasmi ya Upinzan Bungeni, imeibuka na madai kwamba  vigogo wanaotuhumiwa  kugawana fedha  za Escrow   wamenyofoa   baadhi ya karatasi zenye majina yao  ili kuficha  ushaidi  ambapo  wameandaa   propaganda ya kuwahadaa wananchi kuwa ripoti hiyo haijakamilika.
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia ametaja kurasa zilizonyofolewa katika ripoti hiyo kuwa ni zilizobeba mambo ya msingi ambazo ni ukurasa wa 57, 58 na 59.
Watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa mjadala huo utakaorindima wiki hii ili kuwafahamu walioiba fedha za umma na kugawana huku mambo ya msingi kama ujenzi wa shule, madawa hospitalini yakikwama kutokana na tamaa ya watu wachache wasio wazalendo.

clouds stream