Sunday 23 November 2014

KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI


KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI



Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Aidha.Bw Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Katika tukio la mauaji ya  watu 28 ambapo  wapiganaji  wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri  ambao  hawangeweza   kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani ya Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.

clouds stream