Tarehe June 11, 2016
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeshapokea BVR Kit 5000 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu Alphonce Malibiche alipozungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Akizungumzia mashine hizo Alhonce amesema mashine hizo zitatumika katika kuwasajili wananchi kwa hatua zote lengo likiwa ni kuwafikia wananchi ambao hawakujisajili kupiga kura na vijana wanaotimiza umri wa miaka 18.

Naye Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi Rose Mdami amesema NIDA imepanga kutumia za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA.
Ameongeza kuwa baada ya kuhakikisha kila Mwananchi ana Nambari ya Utambulisho, kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili.
Amesisitiza kuwa serikali imekusudia kukamilisha usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote kufikia desemba 31 mwaka huu.