Wednesday, 15 June 2016

Mkapa Ataka Watanzania Waache Tabia Ya Kulalamika



Tarehe June 15, 2016pix1-4

Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa akikata utepe kuzindua kitabu cha kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam
Rais mstaafu wa awamu ya tatu,  Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza katika  mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkapa alisema  watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali badala ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.
“Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali ” alisema Dkt Mkapa.
Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwalimu Julius Nyerere.
Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi.

clouds stream