Prof. Lipumba Akataliwa CUF
Tarehe June 14, 2016
Mwenyekiti wa Zamani wa chama cha CUF Prof . Ibrahim Lipumba aliyetangaza kutengua uamuzi wake wa Kujiuzulu na kurejea kwenye cheo chake cha awali cha Mwenyekiti wa chama hicho, Chama hicho kimemkataa.
Prof. Lipumba ambaye jana alifika makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam na wapambe wake alitangaza nia ya kutaka kurejea kwenye cheo chake kufuatia kujiuzulu Uenyekiti wa Chama hicho mwaka jana kutokana na ujio wa Mwanasiasa Edward Lowassa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema haoni chochote cha maana kwa kuwa sababu zilizomuondoa bado zipo, hivyo amehoji kinachomrudisha ni nini?
Naye Twaha Taslima ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema Katiba ya Chama hicho hairuhusu Kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake ya awali.
Prof. Ibrahim Lipumba ni Mchumi wa kimataifa amezaliwa tar. 6 Juni 1952, Ilolangulu, Tabora, Tanzania amewahi kugombea urais mara kadhaa kupitia Chama cha Wananchi CUF.