Timu ya taifa ya uingereza imetolewa katika michuano ya ulaya
baada ya kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Iceland. Mechi ya uingereza
dhidi ya Iceland ilianza kwa kasi kubwa huku timu ya uingereza ikipata bao la
mapema kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa uingereza Raheem Sterling
kuangushwa katika eneo la hatari na hivyo kuipatia timu yake Uingereza penati.
Penati ya Uingereza ilipigwa na mchezaji Wayne Rooney ambaye hakufanya makosa
na kuweka kambani mpira na hivyo Uingereza ikaongoza kwa bao moja katika dakika
ya 4.
Muda mchache baadae
Iceland walifanya shambulizi na kufanikiwa kusawazisha kupitia mchezaji Ragnar
Sigurdsson katika dakika ya 6.
Muda mchache baada ya Iceland kupata bao walifanya shambulizi
linguine na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 19 kupitia mchezaji Kolbeinn
sigthorsson na hivyo kufanya matokeo kuwa uingerza moja na Iceland mbili.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu ya Iceland ilikuwa
ikiongoza kwa mabao mawili dhidi ya bao moja la Uingereza.
Kipindi cha pili kilianza huku timu ya Uingereza ikifanaya
mashambulizi mengi bila mafanikio. Kocha wa Uingereza Roy Hodgson alifanya
mabadiliko ya wachezaji kwa kuwaingiza wachezaji Jack wilshere, Jamie vardy na
kisha Marcus Rashford bila mafanikio.
Hivyo hadi refa Damir Skomina anapiga kipenga cha mwisho timu
ya Iceland ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili dhidi ya moja la Uingereza na
hivyo kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.
Kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali timu ya
Iceland sasa itakutana na timu ya Ufaransa.