Wednesday, 8 June 2016

Naibu Spika ‘Awamaliza’ Ukawa, Afuta Posho Zao Bungeni


Tarehe June 9, 2016Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.
Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.
Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.
Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na kususia vikao vya Bunge.
Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho.
Aidha, Dk. Tulia  alitoa uamuzi huo baada ya kurejea kanuni za Bunge akitumia kanuni ya tano fasili ya kwanza ya toleo la mwaka 2006 na maamuzi yaliyowahi kufanywa na Spika waliotangulia katika hali kama hiyo.
“Naagiza kwamba wabunge wote wanaojisajili kisha kutoka ukumbini kwa kususia vikao vya Bunge, hawatastahili kulipwa Posho kwa siku zote ambao wamekuwa wakijisajili kuingia ukumbini na kisha kutoka ukumbini,” alisema Naibu Spika.
Uamuzi huo wa Naibu Spika umefuatia hivi karibuni Wabunge wa UKAWA kususia vikao mbalimbali vya Bunge hilo kwa madai ya kutokuwa na imani na Naibu Spika.

clouds stream