Monday 20 June 2016

Nape: Lowassa Alikua Alama Ya Ufisadi CCM


Tarehe June 20, 2016Mwanasiasa Edward Lowassa.
Mwanasiasa Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
Katibu wa Itikadi Na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amesema endapo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa angeendelea kubaki ndani yachama hicho wangekua na mzigo mkubwa wa kuwaaminisha wananchi kuwa CCM si mafisadi.
Akizungumza katika mahojiano mjini Dodoma, Nape amesema Lowassa alikuwa alama ya ufisadi katika chama hicho na alipohamia CHADEMA, CCM ikawa na kazi rahisi ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Lowassa ambaye mara zote amekana tuhuma dhidi yake juu ya ufisadi, aliondoka CCM siku chache baada ya kuenguliwa katika kinyanganyiro cha kuwania  uraisi kupitia CCM na kujiunga na CHADEMA ambapo alipata nafasi ya kugombea nafasi   hiyo kwa mwamvuli wa Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA).
“Watu walikua wanauhusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikua radhi kuchagua hata jiwe lakini si CCM,” alisema.
Nape aliendelea kusema kuwa CCM ilikua pabaya  kwani wananchi waliichoka serikali kutokana na kuingia mikataba mibovu, rushwa, ufisadi na watu waliokuwa wanafanya vitendo vya aibu na kujificha ndani ya chama hicho.
Hata hivyo, Nape alisema Waziri mkuu huyo alikuwa na wafuasi wengi ndani na nje ya CCM ingawa wafuasi hao hawakumsababishia ushindi alipogombea uraisi waTanzania.

clouds stream