Timu ya taifa ya hispania imeaga michuano ya ulaya baada ya
kufungwa na timu ya italia kwa jumla ya mabao mawili bila majibu. Timu ya
Hispania ambayo ndio ilikuwa bingwa mtetezi imeaga michuano ya ulaya 2016.
Katika mechi hii timu zote mbili zilikuwa zinagombani nafasi ya kucheza robo
fainali ya kumbe la ulaya. Katika dakika
ya 33 timu ya Italy ilijipatia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake mahiri Giogrio
Chiellini baada ya kipa wa Hispania, De gea kucheza mpira wa adhabu uliopigwa
na kisha mchezaji Giogrio Chiellini kuumalizia.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya italia
ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza
huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.
Lakini katika dakika
za lala salama mchezaji Graziano Pelle wa italia aliifungia timu yake ya italia
bao la pili, dakika ya 90. Hadi mwisho wa mchezo refa Cuneyt Cakir alipopuliza
kipenga cha mwisho, Italia ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili na kufuzu kwa
hatua ya robo fainali.