Thursday, 16 June 2016

Maalim Seif Ajitoa Sakata La Prof.Lipumba CUF


Tarehe June 16, 2016Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema vikao vya chama ndivyo vitakavyoamua mambo mbalimbali yanayoendelea katika chama hicho na yatakayotokea na vitatangaza maamuzi yake kwa watu wote ikiwemo sakata la aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kutaka kurejea katika nafasi yake hiyo aliyojiuzulu mwaka jana.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Habari na Uenezi CUF, Salim Bimani amesema taarifa hiyo ni kupinga baadhi ya taarifa zinazoendelea katika mitandao ya kijamii ikidai kwamba Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF, Ismail Jussa amemnukuu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif akisema kwamba Prof. Lipumba asahau uenyekiti wa chama hicho.
Amesema taarifa hizo ni za uongo kwani Katibu Mkuu huyo hajatoa kauli hiyo na kudai kuwa hizo ni miongoni mwa propaganda zinazotengenezwa na watu wasiokuwa na malengo mema kwa chama, huku wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya chama.
“Maoni na msimamo wa Katinu Mkuu Maalim Seif ambaye yuko Marekani ni kuwa wanachama wasubiri maamuzi ya vikao vya chama ambavyo ndio vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yatakayotokea ndani ya chama,” ameongeza.
Chama kinatoa rai kwa wanahabari wawe makini sana na vyanzo vya taarifa mbalimbali wanavyotumia ili kupata taarifa sahihi hasa mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kufuata maadili ya uandishi wa habari.
Vilevile chama hicho kinatoa angalizo kwa wanachama wote wa CUF kuwa makini na taarifa wanazopokea na wazithibitishe kwa umakini ili kuwa na uhakika na taarifa hizo na kuepuka kupotoshwa.

clouds stream