Friday, 3 June 2016

UMOJA WA ULAYA WATOA ‘HEKO’ KWA HARAKATI ZA JPM

EUUMOJA wa Nchi za Ulaya (EU) umesema jitihada zimeanza kuonekana za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha lengo namba saba la Mpango wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) linatekelezwa nchini.EULengo hilo limezungumzia suala la upatikanaji kirahisi, kwa bei nafuu na kwa uhakika wa nishati. Hayo yalibainishwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya wa Tanzania na Afrika Mashariki, Roeland Van de Geer wakati wa uzinduzi wa kitabu cha ‘Empowering Tanzania: Energy for Growth and Sustainable Development kinachozungumzia namna ya kuiwezesha Tanzania kuboresha upatikanaji wa nishati kwa maendeleo ya nchi hiyo.

Van de Geer alisema upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa Tanzania ndio ufunguo mkubwa wa maendeleo hasa katika maeneo ya vijijini. “Kitabu hiki kimelenga kutoa maelezo ya jumla kuhusu namna EU itasaidia sekta ya nishati nchini.

Kinazungumzia hatua zilizochukuliwa zamani na zitakazochukuliwa siku zijazo kwa lengo la kuhakikisha lengo namba saba la SDGs linafikiwa,” alifafanua Geer. Alisema umoja huo umekuwa ukitoa misaada katika kuboresha upatikanaji wa nishati kwenye maeneo ya vijijini kupitia miradi midogo ya maji iliyopo katika maeneo ya kusini mwa Tanzania na miradi ya nishati ya jua katika visiwa vya Ziwa Victoria.

Aidha, alisema pia EU imekuwa ikisaidia kuimarisha miradi ya miundombinu ya kusafirisha na kusambaza nishati kwa ajili ya kufikia vijiji kupitia gridi na nje ya Gridi ya Taifa. “Pia umoja huu ni mshirika wa Tanzania katika kufanikisha mageuzi ya msingi ya sekta ya nishati kwa kuongeza ufanisi na uwezekano wa upatikanaji wa fedha,” alisema.

clouds stream