Tuesday 7 June 2016

Serikali Yaondoa Tozo Uhakiki Na Usajili Viwanda Vidogo


Tarehe June 7, 2016mkendao
mkendao
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.
Prof. Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya Wanawake Tanzania.
“Hiyo tozo ilikua ikiwakwamisha baadhi ya wafanyabiashara kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneo yetu ila sasa serikali imeiondoa kabisa,” alisema.
Aidha amesema amewataka wafanyabiashara wilayani na vijijini kuanzisha viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi.
“Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawahimiza wanawake waanze kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure,” alisema Prof Mkenda.

clouds stream