Tuesday 7 June 2016

Mwezi Mtukufu Waligusa Bunge, Lowassa




Tarehe June 7, 2016
Lovely-Mosque-Ramadan-Kareem
Bunge limetengua kanuni zake na kubadilisha muda wa kumaliza shughuli zake kwa lengo la kuruhusu wabunge Waislamu kutimiza wajibu wao wa kiimani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Utenguzi wa kanuni hizo ulipitishwa jana baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenister Mhagama kuomba Kanuni ya 28(4), ambayo kwa ujumla wake inaelekeza kwamba Bunge litaendelea kukaa hadi saa 2:00 usiku.
Mhagama aliomba kanuni hiyo itenguliwe na badala yake, kuanzia siku ya kwanza ya Ramadhani, Bunge lirejee saa 10:00 alasiri kama ilivyo sasa na kuahirishwa saa 12:00 jioni. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote waliokuwamo ndani.
Wakati huohuo Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia alikuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema ameibuka na kuwatakia mfungo mwema waislam wote nchini.
Kupitia ukurasa wake wa facebook. Lowassa ameandika;
“Waumini wa kiislam Tanzania wanaungana na wenzao kote duniani katika kutimiza moja ya nguzo tano Za uislam kufunga Ramadhan.
“Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ni kipindi muhimu sana kwa waislam kuwa karibu na mola wao.
“Kwa niaba ya Mke wangu Regina na Mimi binafsi, nachukua nafasi hii kuwatakia waislam wote nchini,kila la kheri na baraka tele kwenye mwezi huu.

clouds stream