Tarehe June 24, 2016
Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesisitiza kuwa Uingereza inafaa kujiondoa kwa haraka katika muungano huo wakidai kuwa kuchelewa kwake huenda kukazua wasiwasi miongoni mwa mataifa yaliosalia.
Kamishna wa tume ya Ulaya, Jean Claude Juncker amesema kuwa muungano wa mataifa 27 yaliosalia utaendelea kama kawaida.
Uingereza ilipiga kura ya aslimia 52 dhidi ya 48 kuondoka katika muungano wa Ulaya huku waziri mkuu David Cameron akisema kuwa atajiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.
Juncker alifanya mkutano wa dharura na rais wa bunge la Ulaya Martin Schulz, rais wa baraza la Ulaya, Donald Tusk na waziri mkuu wa Ujerumani, Mark Rutte na kutoa taarifa hiyo leo.
Baadaye walitoa taarifa wakisema wanajuta lakini wanaheshimu uamuzi huo wa Uingereza.