Tuesday 10 June 2014

MAUAJI NIGERIA TENA.


Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
140526155053_boko_haram_protests_304x171_reuters_nocredit.jpg hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao.Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwalazimisha wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao katika Jimbo la Borno.
Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Chibok ambako wapiganaji wengine wa silaha waliwteka nyara zaidi ya wasichana 200 wanafunzi Aprili, mwaka huu.
Wakati huo jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo la Borno na Aladawa.
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua dhabiti na wakati mwingine hawapo wakati washambulizi wanaotekeleza uhalifu wao.

clouds stream