Sunday 26 June 2016

Rais Magufuli Awataka Polisi ‘Kuwapora’ Silaha Majambazi


Tarehe June 26, 2016Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Mwigulu Nchemba (kushoto) akiwa na Rais  Dkt John Pombe Magufuli  (katikati) pamoja Mkuu w a Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi wa maboresho ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba (kushoto) akiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli (katikati) pamoja Mkuu w a Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi wa maboresho ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Askari wa Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa wanapambana na majambazi wote wenye silaha na kuwapokonya silaha zao.
Akizungumza katika viwanja vya Biafra kwenye uzinduzi wa Mpango wa Maboresho ya Usalama wa Jeshi hilo katika kupambana na vitendo vya uhalifu vilivyoshika kasi nchini huku matukio mengi ya kiuhalifu yakiripotiwa katika jiji la Dares salaam Rais Magufuli amesema anashangaa kuona Majambazi wenye Bunduki wanavamia na kupora mali za wananchi wakati Polisi  wenye  Bunduki zenye risasi  wapo  huku wakishindwa kuwadhibiti majambazi hao.
“Natoa wito kwa Jeshi la Polisi, mkimuona jambazi ana Bunduki hakikisheni mnampora Bunduki yake”Alisema Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa Polisi yeyote atakayepambana na Jambazi na kumpokonya Bunduki atapandishwa cheo haraka iwezekanavyo kwa kuwa vitendo vingi vya kiuhalifu hufanywa na Majambazi wenye silaha hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Akizungumzia maboresho ya Jeshi la Polisi Rais Magufuli amesema ili maboresho hayo yanaonekane yana tija ni lazima vitendo vya uhalifu vipungue kutoka  kuanza kwa mfumo huo ambao umeonesha kubadilisha utendaji wa Jeshi la Polisi hapa nchini.
Kwa upande wa Vitendo vya uhalifu Rais Magufuli amesema mwaka 2012 vitendo vya uhalifu vilikuwa 4410, mwaka 2014 vilikuwa 8015, na Mwaka 2015 vitendo vya uhalifu   viliongezeka hadi kufikia  8804.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu amesema Jeshi la Polisi limeboresha kitengo cha kupokea taarifa kutoka kwa wananchi ambazo zitafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Mangu amewataka wananchi kupiga namba 111 au 112 ili kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu ambapo baada ya kutoa taarifa jina mtoaji litakuwa siri ili mtoa taarifa  asije  kupata  shida  ya usalama  wake.Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi Jukwaa kuu kwenye viwanja vya Biafra leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi Jukwaa kuu kwenye viwanja vya Biafra leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi Jukwaa kuu kwenye viwanja vya Biafra jana.

clouds stream