Monday 4 July 2016

Mabasi Ya City Boy Yaua 25 Singida


Tarehe July 5, 2016pic+ajali
pic+ajali
Kamanda wa polisi mkoa singida Thobias Sedoyoka
Watu 25 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa leo baada ya mabasi mawili kugongana huko Maweni wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa singida Thobias Sedoyoka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo inahusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea Dar es salaam kwenda Kahama na basi T 247 linalotoka Kahama kwenda Dar es salaam yote ya kampuni moja CITY BOYS.
“Mabasi hayo yamegongana uso kwa uso na kuua abiria 25 papo hapo na kujeruhi wengine,” alisema.
Kamanda Sedoyoka alisema idadi zaidi ya vifo itaendelea kutolewa.

clouds stream