Thursday 13 March 2014

MICHAEL JORDAN KATIKA PICHA ZA KIHISTORIA.

Michael Jordan akidunk katika mchezo wa nne wa msimu akicheza dhidi ya Detroit mwaka 1991. Chicago Bulls kipindi hiki ilifanya malipizi kwa kuwatandika Pistons na Detroit mfululizo.

Jordan akitupia mchomo wa ushindi dhidi ya  Utah Jazz katika mchezo wa 6 mwaka 1998 akiiwezesha timu yake kutwa ubingwa. Jordan aliweza kumkwepa kwa ustadi mlinzi Bryon Russell na kuputia kikapu.
Jordan akiwa anadunk kwene shindano la mwaka 1998 katika Slam Dunk competition. Style hii ya kudank ilimpatia Jordan ushindi kwa mara ya pili akimpita Dominique Wilkins.
Michael Jordan akiwa na mama yake Deloris baada ya kuwapiga Utah Jazz mwaka 1998. katika sekunde 41.9 Jordan alifanya layup, aliiba mpora kutoka kwa Karl Malone na kufunga kikapu kilichowapa tofauti ya point 3 mbele ya wapinzani wao.
Jordan akijaribu kumzuia mtaalam Magic Johnson katika mchezo wa 5 mwaka 1991. katika siku hii, Jordan alifunga point 30 na kutoa pasi za kikapu 10.
Mwaka 1987, Jordan akiwa amezingukwa na watoto wakiwania kupata japo sahihi ya mchezaji huyu maarufu.
Skottie Pippen akimsaidia Jordan kutoka nje ya uwanja akiwa amechoka na akiwa anaumwa mwaka 1997. Jordan alicheza mchezo huu akiwa anaumwa tumbo na alifunga pointi 38 kabla ya kuanguka kwa muda kwenye mchezo huu.

Kocha mkuu wa chicago bulls Doug Collins akitoa maelekezo kwa Jordan katika mchezo dhidi ya Cleveland. 
Jordan akiwatia moyo wachezaji wenzake wa Wizards akiwa kwenye bench Octoba 2001. Jordan alitangaza kurudi kwake uwanjani septemba 25 mwaka huo.

Jordan akipaa kuelekea kwenye rim akiwapa mateso makubwa Philadelphia 76ers
Jordan akiwania mpira dhidi ya Kevin Johnson na Charles Barkley akitafuta pointi 3 muhimu . Barkely alifanikiwa kumpiku Jordan na kua mchezaji mwenye thamani (MVP) katika msimu huu.
Jordan akiwa katika kupigwa picha mwaka 1987 ya kuwekwaa kwenye gazeti la Action.
Jordan akimpita Charles Barkley mwaka 1991 huku ulimi ukiwa nje. Baada ya hapa, Jordan aliomba watoto wasijaribu kufanya hio kwani ni hatari iwapo waanguka.
Jordan akichezea timu ya olimpiki ya USA na kuisaidia timu yake kuchukua medali ya dhahabu mwaka 1984.
Jordan akidunk. Hapa maneno hayastahili kuongezwa sababu sura yake inasema yote.

clouds stream