Saturday 20 September 2014

Everton yaanza vizuri Europa


Everton yaanza vizuri Europa

Michuano ya UEROPA maarufu kama UEFA ndogo imeanza vyema ambapo Everton ya England  ilianza kwa kuisambaratisha Wolfsburg ya Ujeruman magoli 4 - 1.
Timu ya Tottenham walikuwa wagen wa Partizan Belgrade ya Serbia ambazo zitoka sare ya kutofungana huku Villarreal ikatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach pia ni ya Ujeruman.
Nayo FC Red Bull Salsburg ya Austria ikaishia sare ya 2-2 dhidi ya Celtic.
Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Fiorentina ambayo ilibanjua Guingamp ya Ufaransa kwa jumla ya 3-0, nayo Zurich ikapokea kipigo cha mabao 2-3 kutoka kwa Apollon Limassol ya Ugiriki
Matokeo mengine ni mechi ya Brugge ya ubeligiji ilitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Torino ya Italia na Dynamo Kiev ikaifunga Rio Ave ya Ureno magori 3-0.

clouds stream