Monday 16 February 2015

Hotel ya Kendwa Rocks yateketea kwa moto visiwani Zanzibar

Hotel ya Kendwa Rocks yateketea kwa moto visiwani Zanzibar


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole mwakilishi wa Hotel ya Kendwa iliyoteketea kwa moto Zanzibar.
Hotel ya Kendwa Rocks  iliyopo katika kijiji  cha Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja imeteketea kwa moto kufuatia hitilafu ya umeme na kupelekea  sehemu kama za duka, ukumbi wa burudani zimeteketa kabisa.
Kwa mujibu wa wahudumu wa Hotel hivyo wameiambia Hivisasa Blog kwamba moto huo ulizuka na kuenea kwa kasi kutokana na upepo mkali majira ya saa nne asubuhi jana  ambapo hasara ya  takribani bilioni moja inasadikiwa kupatikana kutokana na moto huo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ametembelea katika eneo la tukio kujione hali ilivyo.  Mara baada ya kutembelea  amewapa pole wamiliki wa hotel hiyo kufuatia hasara kubwa waliyopata.

clouds stream