Monday 16 February 2015

Afrika Kusini yapiga marufuku wageni kumiliki Ardhi

Afrika Kusini yapiga marufuku wageni kumiliki Ardhi

Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini. Mbali na hilo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kuwagawia wananchi.
Ardhi bado ni suala linalozusha hamasa nchini humo – ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi – zimeacha  asilimia  kubwa ardhi  mikononi mwa wachache, hasa wazungu.
Hata hivyo, tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.

clouds stream