Monday 15 September 2014

OKWI ALIVYO WA INGIZA YANGA MJINI


OKWI EMMANUEL  
In Summary
Moja ya mashauri yaliyokuwa yakijadiliwa hapo juzi ni kesi iliyofunguliwa na× Yanga kupinga uamuzi wa mshambuliaji wao× Okwi kujiunga na Simba wakati bado akiwa na mkataba na klabu hiyo.
NI Jumapili majira ya saa 9:30 alasiri tulivu ambapo wajumbe wa× Kamati ya Sheria na× Hadhi za Wachezaji kutoka× Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walianza rasmi kikao kujadili mashauri kadhaa yaliyowasilishwa katika kamati hiyo ingawa× Yanga na Okwi walifika eneo la hoteli ya× Colosseum saa 4 asubuhi.
Moja ya mashauri yaliyokuwa yakijadiliwa hapo juzi ni kesi iliyofunguliwa na× Yanga kupinga uamuzi wa mshambuliaji wao× Okwi kujiunga na Simba wakati bado akiwa na mkataba na klabu hiyo.
Kamati hiyo iliketi kuanzia muda wa saa 9.30 alasiri hadi saa 12:15 jioni (dakika 165) ambapo pande mbili yaani walalamikaji (Yanga) wakiongozwa na× Mkuu wa klabu hiyo× Njovu na mwanasheria wao× Mapande na mlalamikiwa (Okwi) akiwa na mwanasheria× Ndumbaro, ambaye alimwakilisha mwanasheria wa Okwi, Edgar Aggaba waliondoka ukumbini hapo.
Hali ilivyokuwa
Kamati ilitoa fursa kwa Yanga kuwasilisha vielelezo vyote juu ya hoja zao ambapo Mapande na Njovu walifanya hivyo kabla ya baadae Okwi na Ndumbaro kuambiwa wapeleke utetezi wao.
Kamati ilichukua muda wa saa mbili kusikiliza pande hizo mbili na kupeana mapumziko mafupi kabla ya kurejea tena kumalizia mashauri hayo. Hata hivyo utulivu uliendelea kutawala hotelini hapo huku wajumbe wakiingia na kutoka katika chumba cha majadiliano.
Pande zote mbili zilionekana kuwa na matumaini ya kushinda kesi hiyo lakini baadaye upande wa Okwi na Ndumbaro ulionekana kuwa na mashaka kuwa endapo Kamati hiyo itaamua kutoa uamuzi wake kwa kupiga kura basi ‘ingekula kwao’.
Wasiwasi huo ulitokana na dhana ya kwamba kamati hiyo ina wajumbe wengi ambao ni wanachama wa Yanga akiwemo mwanasheria Iman Madega aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga na Abdul Sauko aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo huku upande wa Simba ukidaiwa kuwa na wajumbe wawili tu mmoja wapo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.
Ukumbi wabadilishwa
Awali hukumu hiyo ilipangwa kufanyika katika ofisi za TFF kama ambavyo wajumbe walitangaziwa awali lakini kwa hofu ya kutaka utulivu hasa kwa lengo la kutaka kuwakimbia makomandoo wa Simba na Yanga ukumbi huo ulibadilishwa haraka na kupelekwa katika hoteli ya Colosseum ambako ndiyo kila kitu kilimalizika huko.
TFF baada ya kufika Colosseum walikosa ukumbi wa kufanyia mkutano baada ya hoteli hiyo kujaa hawakuwa na mbadala mwingine zaidi ya kutafuta chumba na kupatiwa chumba namba 201 ghorofa ya pili ambako ndipo kila kitu kilifanyika hapo.
Hoja ya Yanga yadunda

clouds stream