Saturday 20 September 2014

Maelfu Wajitokeza Kumsindikiza Freeman Mbowe Polisi Alipoitwa Kuhojiwa Kuhusu Kauli yake ya Maandamano

MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi hii wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuelekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.

Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

Katika tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika makao makuu hayo ya polisi

clouds stream