Saturday 7 February 2015

Cannavaro aomba radhi kwa ‘kumbusu’ afande

Cannavaro aomba radhi kwa ‘kumbusu’ afande

Nadir Haroub 'Cannavaro' Nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa 'Taifa Stars'
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’
Nahodha wa Yanga na timu ya ‘Taifa Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ amemuomba radhi askari aliye mkumbatia na kumbusu wakati akishangilia kufunga goli wakati timu yake ilipo cheza na Coastal Union Jumatano iliyopita kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Cannavaro alifunga bao hilo pekee kwa timu yake katika dakika ya 11, bao lililoipa Yanga ushindi wa goli 1-0, baada ya kufunga goli hilo Cannavaro alikimbia huku akishangilia na kwenda kumkumbatia askari huyo na kumbusu.
Cannavaro alisema alimuomba msamaha askari huyo muda mfupi baada ya mechi hiyo kumalizika, ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya kwa kufanya kitendo hicho.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali na kumsamehe kwa yote yaliyotokea kwani hakutarajia hali hiyo kutokea na ilikua ni furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo,” Cannavaro alisema.
“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya,
nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisisitiza.

clouds stream