Wednesday 17 February 2016

Mchezaji Amuua Mwamuzi Baada Ya Kulambwa ‘Red Card’

Mchezaji Amuua Mwamuzi Baada Ya Kulambwa ‘Red Card’

Tarehe February 17, 2016
160217103805-red-card-ref-hand-exlarge-169
Mwamuzi mmoja nchini Agentina amepoteza maisha baada ya kuuawa na mchezaji aliyemtoa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNN, Cesar Flores, alikuwa akichezesha pambano mjini Cordoba, takriban kilomita 700 Kaskazini Magharibi mwa Mji Mkubwa wa Buenos Aires, pale ambapo alimwonyesha mchezaji ambaye hakuwa na silaha kadi nyekundu.
Baadae mchezaji huyo alichukua bastola ndani ya begi lake na kurudi uwanjani na kumpiga mara tatu mwamuzi huyo mwenye miaka 48, katika maeneo ya shingo, kichwa na kifua.
“Yote yalitokea wakati wa mechi,” chanzo cha polisi kilisema.
“Hatujui nini kilitokea kwa mwamuzi, lakini mchezaji alikuwa na hasira na kwenda kuchukua silaha yake na kumuua mwamuzi,” kilizidi kusema chanzo hicho.
Mtuhumiwa bado yupo mtaani na hajakamatwa.
Katika tukio hilo, mchezaji mwingine alijeruhiwa vibaya sana lakini inaaminika kuwa majeraha yake hayatatishia uhai wake.
Amerika ya Kusini imekuwa ikikumbwa na visa vya kutisha katika viwanja vya soka ambapo mwaka jana mwamuzi mmoja nchini Brazil alimnyooshea bastola mchezaji aliyemdhihaki, na mwaka 2013 mchezaji mmoja alichomwa kisu na mwamuzi baada ya kuzuka vurugu. Mwamuzi huyo baadaye alitekwa nyara na mashabiki ambao walienda kumtesa vibaya kabla ya kupigwa mawe hadi kufa.

clouds stream